SELF HEALING (UPONYAJI BINAFSI PART ONE)

SELF HEALING (UPONYAJI BINAFSI )

SEHEMU YA KWANZA
🔥Kuna aina ya matatizo hasa Yale ya kisaikolojia.yanapompata mtu huwa inakuwa vigumu Sana kuyashughulikia

Mfano
➖Usaliti
➖Kufukuzwa kazi
➖Kusemwa vibaya
➖Kuumwa ugonjwa unaokutisha zaidi
➖Kutokea kwa jambo linalokuogofya Sana

Mara nyingi mambo Haya yanapotokea husababisha *Msongo wa Mawazo,*Dipression,*Kudhoofika kwa mwili,*Baadhi ya viungo kupata ulemavu(kulemaa),*Kupooza*na kwa wanandoa  hali hii inaweza kupelekea hata kushindwa kufanya tendo la Ndoa*

*➖Unaweza ukakutana na mtu amepooza ukajua aliugua kumbe ni kwa sababu ya msongo wa mawazo*

👉🏼Mtu anapofika katika level hii ya umio la moyo(broken heart) sio rahisi Sana kupona na hatimaye kurudi katika hali yake ya kawaida.

*👉🏼Kuna wengine huwa hadi wanachanganyikiwa na kuanza kuzungumza peke yao*


*Mfano*
Uwe na uhakika kabisa katika kitabu cha 1samweli 1:3.....Hana aliyekuwa Hana mtoto ...ilimpelekea kuumia Sana moyoni,

Walokole wengi wanadhani aina ya maombi aliyokuwa anayaomba Hanna hadi mumewe akawa anamwambia amelewa ...yalikuwa ni ya Rohoni sana....nikwambie tu kuwa ...yawezekana maombi Yale yaliambatana na kupaniki Sana...na unapoomba ukiwa umepaniki ...usitegemee kugusa Point za msingi kwenye maombi

Unapopaniki ukaanza kuomba ...kuna hisia huwa zinakujia na hizi hisia Kama hauko Rohoni unaweza kuhisi ni Roho mtakatifu kumbe ni Hisia za maumivu tu ya huyu mtu

Mifano ya hisia anazoweza kuzionesha mtu akidhani yuko Rohoni kumbe ni Brocken heart)
👉🏼Kulia Sana kwa uchungu
👉🏼Kuzungumza peke yako muda mwingi
Kama Hana..(1Samweli 1:10)
"Na huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake,akamwomba Bwana Akalia sana"

✍️sasa sio kila anayeomba na Julia sana Mbele za Mungu anakuwa yuko Rohoni...kuna wengine wanalia kwa sababu ya *majeraha ya moyo*

Na wakati Mwingine ..ili aweze kupona katika tatizo lake...asingehitaji maombi,Ila angehitaji *self healing*

✍️Kazi ya maombi ni kuruhusu nafsi yako Iwe karibu na Roho wa Mungu,akupatie ufunuo wa wewe utokaje pale ulipo...Sasa kuna watu wanalia kwa uchungu halafu wanasingizia kuwa ndio maombi ...nayo...na kwa bahati mbaya ...Mungu huwa hajibu maombi ya uchungu usiozaliwa na Roho wake...katu hatakuja kufanya upuuzi huo

🔥 Unahitaji kutumia *self healing* baada ya kuomba...nakwambie kweli inaponya...binafsi imenisaidia sana.

*🔥sio kila tatizo linapona kwa maombi,kuna matatizo Mengine yanapona kwa Kufanya self healing...Ila kabla ya kuanza huu mchakato wa self healing utahitaji maombi tena yasiyo ya uchungu...ambayo yatakujenga nafsi yako uweze kusikiliza sauti ya Mungu...ili uingie katika utendaji wa kujiponya nafsi yako mwenyewe*

*KWANINI UNAHITAJI SELF HEALING?*
1.kuna siku utaumizwa ukiwa peke yako .hatakuwepo mtu wa kukufanyia counselling....hivo Kama usipojifunza self healing utakufa kwa mawazo

2.Mungu amekuumba uwe na uwezo wa kujiponya mwenyewe self healing na ndio maana ukiumwa Kama Imani yako iko vizuri hata bila dawa unao uwezo wa kupona,maana unapokuwa hauna mashaka (unapisupress mashaka) unatengeneza au Una activate mfumo wa self healing kuanza kuchakata uponyaji wako mwenyewe

3.Self healing inakusaidia kuwa karibu na Mungu zaidi maana hapo ni Kati ya wewe na Mungu tu

4.Self healing huwa inasaidia sana kujenga Imani kwa Mungu na kuto kuwategemea wanadamu

5.Self healing ni Ishara tosha ya kuwa uko kamili na umeumbika kikamilifu na hauna mapungufu katika mfumo wa akili yako

6.Self healing ni njia ya pekee isiyohitaji gharama kubwa..

7.Self healing inakutengenezea kinga ya kudumu dhidi ya tatizo Kama hilo ..hata likitokea baadaye

8.Self healing inakuzoesha kutoumia hata Kama utapitia wakati mgumu zaidi

9.Self healing hujenga ujasiri

*10.Self healing Hujenga Imani binafsi*

Njoo jifunze ..ukuze nafsi yako

🇹🇿Mwal.Chavala PM Ezekia

©️Ogschavala@gmail.com
+255677904755

©️Jiunge nasi kwa kubonyeza link hii
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA

©️Download application yetu ya online gospel sermons kutoka play store upate masomo yetu ya kila siku

Nenda google play kuipata

©️Fuatilia page yetu Facebook..Gospel Sermon Ministries na Instagram..Mwal..ezekia_Chavala official.

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.