MAJI YANAPOZIDI -UTAZIDI KUPATA NGUVU YA KUELEA
♨️Ni katika siku ya leo tena ambayo Mungu ametupatia ili tumwabudu
♨️Kuna kitu kizuri nimejifunza leo ,naomba pia na wewe upate japo sehemu
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Mwanzo 7:18
*18 Maji yakapata nguvu, yakazidi sana juu ya nchi; na ile safina ikaelea juu ya uso wa maji.*



🔥Nilikuwa napitia kitabu cha Mwanzo ile sura ya sita na Saba,kuna vitu Bwana amenisemesha nimeshangaa Sana

1️⃣Unapokuwa na Mungu( Ndani ya Yesu) unakuwa na usalama wa kutosha,
✍️Kwa kadri mafuriko yanavyozidi kujaa zaidi,ndivyo ambavyo yanakupatia nguvu za kuelea zaidi


➖kwa wale wataalamu wa Majini na vyombo vya usafiri wanasema,Meli kubwa huwa inasafiri kwa raha na utulivu mzuri zaidi sehemu yenye kina kirefu baharini
✍️Kina kirefu maana yake Maji yake ni Mengi Sana

Sasa Ukirudi katika mstari tuliosoma;

♦️Kabla maji hayajaanza kuwa mengi,Ile safina haikuweza hata kuelea,

♦️Kabla maji hayajaanza kuwa Mengi,Uwezo wa ile safina haukuonekana💥💥

♦️Kabla Maji hayajaanza kuwa Mengi,Watu walimdharau Sana Nuhu kwa sababu maana ya ile safina haikuonekana wakati huo

Nuhu alionekana Kama ametengeneza kituko Fulani tu


2️⃣Maji yalipoanza kuongezeka ndipo;
♦️Safina ikapata upenyo wa kuanza kuelea
♦️Yalipoongezeka zaidi ..ikaanza kuelea vizuri zaidi
♦️Wale watu waliomcheka Nuhu,walianza kumkimbilia pale safina ilipoanza kuelea na wakati huo mvua kubwa inanyesha nje hakuna mfano wake


3️⃣Maadamu tu uko na Mungu,matatizo,majaribu na adha yeyote inapokukuta( mafuriko) jua kuwa ni kwaajili tu ya kukufanya uelee vizuri

Na kuanzia hapo;
💥Uwezo wako utaanza kuonekana..maana hauwezi kuonekana Kama mwenye uwezo Kama hujapimwa katika misukosuko

💥Maji yako yanapoongezeka ndipo pia utukufu wako utaongezeka(Bwana atakufunua katikati ya mataifa)

💥Hatuwezi kujua wewe ni hodari hadi pale tutakapoona unaeleea juu ya maji wakati huo mafuriko yameongezeka Sana

🔥Nakuona Jinsi ambavyo siku ya leo utaacha kukata tamaa unapopatwa na changamoto
🔥Nakuona jinsi ambavyo hutalia tena unapoona mafuriko yanaongezeka ,Bali utaanza kuelea na kuonesha uwezo wako kuwa majaribu na changamoto zako ni kukutengenezea momentum uweze kung'ara zaidi


NB;Dhahabu ili Iwe safi ni lazima ipitishwe kwenye Moto

*Hesabuni kuwa ni furaha tele muangukiapo katika majaribu*
Nikutakie ushindi katika kila jambo siku ya leo

Bwana akuinue na kukutia Nguvu


Mwal.Chavala PM Ezekia

Online Gospel Sermons

+255621029725
Ogschavala@gmail.com

Kujiunga na kupata mafundisho haya bure,bonyeza link hii


https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.