*UMUHIMU WA KUFUATA KATIBA (NENO)*
👉🏼Ukiona unasoma sermon hii,jua na wewe Bwana amekuteua kujiunga na siku ya leo..Jina lake Libarikiwe
🌹wananchi wengi hawajui faida ya kufuata katiba ya Nchi yao,ndio maana kuna wakati wanajikuta hawazijui wala kuzitambua haki zao za Msingi


📌katika upande wa Imani pia...unapoifahamu katiba(mkataba wako na Mungu) maelekezo ya Mungu kwa viumbe wake( statement ya Mungu kwa wamchao)- kuna vitu utaanza kuvipata bila usumbufu wowote na bila kutumia Nguvu kubwa.

*Nifwatilie kwa makini*
1️⃣Kila kampuni inayozalisha bidhaa,huwa inatoa warranty na guarantee kwa watumiaji kwaajili ya kulinda jina la kampuni yao

✍️Kuna wakati watakwambia Kama ukiona bidhaa imekusumbua basi uirudishe kwa watengenezaji waweze kukurekebishia....tena kwa gharama za kwao

✍️ila huwa wanatoa masharti kuwa...usipeleke kwa fundi mwingine 😅😅ukipelekea kukorokochoa kwa mafundi wengine kampuni haitahusiaka na uharibifu wa bidhaa waliyokuuzia

*Tunajifunza nini?*
🌹Mungu alipokuumba wewe,ni Kama product(bidhaa yake)
🌹Unapoishi maisha ya shida na kutangatanga unamtia aibu yeye( yaani unamfanya reputation yake(jina lake Liaibishwe)

*Mwanzo 1:2-kuumbwa kwa mfano wa Mungu maana yake anataka uoperate katika mfumo wa Kimungu...Unapofanya kazi chini ya viwango ,jina lake linatukanwa( you ruin his reputatio)*

2️⃣Mapenzi ya Mungu ni wewe umuwakilishe yeye hapa Duniani..

🌹sasa ni hatari Sana Balozi wa Mungu Duniani...anaishi maisha ya kitumwa..na hofu na kuteswa..kiufupi anakuwa Kama mtumwa
📌unapokuwa balozi tunategemea mambo yafuatayo kutoka kwako

➖Unamuwakilisha aliyekutuma( ulikotoka)
➖Vile unavoonekana ni picha ya yule aliyekutuma( unayemwakilisha)
➖hutumii gharama zako mwenyewe ..Bali unatumia gharama za aliyekutuma
➖Huduma zote unazozitoa ni kwaajili ya aliyekutuma


*🌹Basi tu wajumbe wa Kristo kana Kwamba Mungu anasihi kwa Vinywa vyetu....nawaomba kwajili ya Mungu Mpatanishwe.....*

Wajumbe ni mabalozi😅😅😅

✍️Ukiona balozi mchafumchafu...maana yake nchi anayoiwakilisha iko hoi Sana...

✍️ukiona balozi ni masikini ,jua anayemuwakilisha ni masikini zaidi

✍️ukiona balozi Hana nguvu ya kusema na kuamua ..jua anakotokea ni utumwani tu

✍️ukiona balozi ..hajielewei elewei ..jua anayemwakilisha ndio kabisaaa shida tupu

3️⃣Mungu anataka tufanikiwe kwaajili ya reputation yake mwenyewe

🌹yani unapofanikiwa ...Mungu ndicho anachokitaka..ili jina lake litukuzwe..
( hakuna Manufacturer wa bidhaa anayependa bidhaa yake isisifiwe kuwa bora) maana anajua bidhaa yake ikitukanwa..basi jina la kampuni yake liko hatarini😅😅

🌹ukielewa jambo hili...hutaanza kuomba maombi ya Baba naomba nifanikishe ...hapana...utaanza kutamka maombi ya kumsifu na kumtukuza Mungu kwa kukufanya mkuu,uliyebarikiwa Sana na mwenye mafanikio makubwa..kwaajili ya utukufu wa Mungu


4️⃣Kuna masharti ya kufuata ili mwenye bidhaa aweze kukupatia warranty na garrantee ya kufanikiwa

Yani Neno la Mungu.

🌹usiposoma na kuelewa neno la Mungu,hakuna namna utajua terms of condition katika mkataba wa wewe na aliyekuumba wa kufanikiwa kwako

Joshua 1:8

*8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.*

Sasa fuata masharti ili kusudi umuwajibishe aliyeyaweka kwa urahisi


Ameikuza ahadi yake kuliko jina lake..Sasa..unapoingia kwenye maombi ukiwa unajua ahadi yake katika Neno...unampatia wakati mgumu wa kuona anatakiwa kuitimiza..hakuna namna maana asipotimiza ataonekana ni muongo


Fuata masharti ...na mkataba unavosema...ili upate maneno ya kumwendea kwa hoja nzito Mungu wetu

*Kwa hakika atakujibu kwaajili ya Jina lake...sio kwaajili yako...remember this😅*

Nikutakie siku njema

Chavala PM Ezekia
Online Gospel Sermons

+255621029725

https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.