UNAPOKUWA KATIKA HOFU

*UNAPOKUWA KATIKA HOFU!!!!*
Ni matumaini yangu kuwa Bwana amekuamsha salama siku ya leo,Hongera Sana kupata nafasi hi I
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖




♦️Dunia imejaa hofu nyingi,kila siku kunapokucha tunakutana na aina mbalimbali za Hofu
✍️Watu wanaugua magonjwa yasiyokuwa na tiba na akishaugua anapata *Hofu ya kifo*

✍️Watu wanagombana Sana katika familia zao  na hili linazaa Hofu ya *kuvunjika kwa familia*

✍️Watu wanafanya makosa ofisini kwao na hili linazaa *hofu ya Kutumbuliwa*

✍️watu wanahitimu vyuo vikuu kila mwaka na wakiangalia mtaani hakuna ajira ,hili linazaa *Hofu ya kukosa kazi na kupoteza muda shuleni*


✍️Watu wanakaribia kustaafu,na hakuna msingi wa maisha walioufanya,hili linapelekea *hofu ya kustaafu bila kuwa na vitega uchumi*


✍️Ndugu zetu wanasafiri kwenda Nchi za nje,na wanaporudi tunasikia nchi wanazotoka kuna janga kubwa la Corona 19,hii inatuletea *hofu ya Corona*

✍️pesa inakuwa ngumu kupatikana kwa urahisi,wafanyabiashara na wafanyakazi wanalia uchumi kwao ni Kama hauendi,hii inaleta *hofu ya Umasikini*

⛔Utagundua kuwa Hofu imetanda dunia nzima,watu wako katika mikiki mikiki ya kutafuta maisha asubuhi hadi jioni,wakati huo wako na stress zisizokoma


❗❗❗❗❗❗❗❗❗❗❗❗❗❗❗❗❗
Ni nani atakayemsaidia na kumtuliza hofu hizi mwanadamu huyu?

➖Kuna vitu ambavyo hats Kama utaviogopa Sana,hauna uwezo wa kuvibadilisha,Ila Mungu pekee anao uwezo wa kubadilisha matokeo

*Zaburi 34:4*
 * *4Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote*

Majibu yako hapa
1️⃣Mtumaini Bwana kwa Moyo wako wote ,wala usitegemee akili zako mwenyewe

2️⃣Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

3️⃣Wamtumainio Bwana ni Kama Mlima sayuni,ambao hautatikisika wakaa milele yote

4️⃣Hutaogopa hofu ya mchana,wala mshale urukao usiku😅😅😅😅😅😅😅😅😅😅


Hizi ni zaburi chache nilizoamua kukutamanisha asubuhi ya leo ,Kama wewe hausomi Neno la Mungu,bila Shaka ni lazima utapaniki Sana..na utapata hofu Sana

Ila kwa wanaolicha Jina la Bwana ,Jua la haki litawazukia,wataenda wakiimba kwa furaha za shangwe

Maana Wamngojao Bwana watapata nguvu mpya ,wataruka juu kwa mbawa Kama tai ,wala hawatachoka♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️♨️


Nikutakie siku njema
Mwal.Chavala PM Ezekia

Online gospel Sermons
+255621029725

4 Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.

Kupata masomo haya ..bonyeza hapa😅

https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.