MATOKEO YA UTUKUFU WA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO
2-MARCH 2020-Mwal.Chavala Pm Ezekia
*Theme;Matokeo ya kuwa na utukufu wa Mungu katika maisha yako*
🤝🏼Hongera sana kwa kufika siku ya leo tena..na hongera kwa kumaliza weekend salama
👉🏾Katika mtiririko wa somo hili tumeona matokeo mawili ambayo ni
1⃣Kung'ara na kupata kibali
2⃣Kubadilishwa kwa historia mbaya ya maisha yako
Na leo tutaenda kujifunza kitu cha tatu kinachotokea unapokuwa na utukufu wa Mungu
*3⃣KUVUNJIKA KWA MIPAKA YAKO*
Utukufu wa Mungu unapokuzukia na kukufunika,mipaka uliyopo haitakuwa na uwezo wa kukushikilia tena
💥Kilichowatoa wana wa Israeli Misri kwenda kanani ni utukufu wa Mungu( mipaka haikuweza kuwazuia
➖Bahari haikuweza kuwazuia
➖Farao na Jeshi lake ..hakuweza kuwashikilia tena
➖Ule utumwa haukuweza kuwa sehemu yao
*Sasa angalia sana ,kila mtu ambaye Utukufu wa Bwana ulimfunika..utaona kuna namna mazingira yake ya awali yalimtapika akajikuta ameenda mazingira mapya yanayoendana na utukufu mpya*
🎯Kumekuwa na maswali mengi sana hasa kwa upande wa watumishi wa Mungu na waimbaji,kwamba inakuaje mtu anaanza kufanya uimbaji akiwa mbeya..halafu anapoanza kupata kibali katika jamii anahamia Mjini( namaanisha Dar😅😅)
Majibu ni haya hapa ..na hili jambo liko kitheolojia kabisa
Mungu anapokuinua..na mazingira pia huwa yanahusika kukubeba..sasa ikitokea utukufu unaoubeba ni mkubwa kuliko mazingira uliyopo...mazingira huwa yanapasuka( yanavunja mipaka iliyokuziba usichanue)
➖Lengo kubwa huwa ni kukufanya uangaze eneo kubwa zaidi na lenye watu zaidi kulingana na kiwango cha utukufu ambao Mungu ameuweka ndani yako
🤔🤔eneo unaloishi ( mazingira unayoishi sasa ni matokeo ya kiwango cha utukufu ulioubeba )😅😅
💥sasa usianze kunikasirikia hapa
Niseme tu UTUKUFU aliokuwa ameubeba Yusufu..ulimlazimu aende mjini Misri ili akawe waziri mkuu
💥Utukufu alioubeba Daudi ..ulimlazimu atoke msituni kuchunga kondoo aende akawe mfalme mjini
💥Utukufu alioubeba Bwana Yona baada ya kutubu ndani ya tumbo la samaki ulimlazimu atoke nje ..ya tumbo la samaki..yani atapikwe na yule samaki💪🏼💪🏼💪🏼💪🏼
💥Huwezi kubeba utukufu wa Mungu mkubwa katika maisha yako..halafu Mungu huyohuyo akuache kwenye eneo ambalo halikutoshi😅😅
Soma Isaya 60;1
*1 Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia.*
Unaondoka ulipo na kuelekea sehemu nyingine kutokana na namna mazingira yanavokuwa na uwezo wa ku accomodate utukufu ulioubeba
🤔usishangae kuona mtu yuko porini..anapoanza kuchanua anahamia mjini
Hii ni formula ya kiutukufu💥💥
Isaya 60:3
*3 Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.*
Kwa tarifa yako..wafalme watakujia..sasa wafalme au watawala mara nyingi hupatikana katika miji mikubwa na maeneo yenye umati wa watu wengi..
Capital city haiwezi kuwa porini
Unapobeba utukufu mkubwa..ni obvious unahamishwa kupelekwa kwenye population itakayoweza kuhudumiwa kwa utoshelevu..na hapo ndipo utakutana na wafalme💥💥
Come on...wafalme hawapo porini💪🏼💪🏼
Daudi kule porini alikutana na simba na dubu na wanyama wa porini..ila Mjini ndiko alikokutana na wafalme ..akina Sauli na wengineo
Kwa wale wanaolia wakiwa maporini..nataka siku ya leo nikufundishe kanuni hii
Tafuta utukufu wa Mungu ukufunike kwa wingi..maana utukufu utakaoubeba katika maisha yako..utaamua uishi wapi😅😅💪🏼💪🏼
Nakutakia siku njema
Kwa maswali na maoni tuandikie
Ogschavala@gmail.com
Call+255677904755
+255621029725
Kujiunga na ogs watsap..bonyeza link hii bure ..upate masomo haya kila siku
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments