UNAWAZA NINI??
Na.Mwal.Chavala..Pm Ezekia.
Hivyo ulivyo wewe leo ni matokeo ya vile unavyotafakari muda mrefu
👉🏼Ukiona mtu ni Jambazi...tafsiri yake kichwa chake kinawaza Sana wiziwizi na ujambazi tu
👉🏼Ukiona mtu ni mchawi,muda mwingi anawaza kuwangawanga tu
👉🏼Ukimuona mtu ni jasiri,katika kichwa chake anawaza ushindi ushindi tu
👉🏼Ukimuona mtu ni goigoi,kichwani kwake Hana chumba cha ukakamavu
👉🏼Na ukimuona mtu amefanikiwa ..kichwani kwake anawaza kufanikiwa zaidi
✍️Kila eneo ambalo unajiona upo leo ni matokeo ya
➖Taarifa➖Tafakari➖Tafakari za kina➖Character(tabia)➖Imani
Hii ni chain ya kuzalisha kila aina ya Imani..hapa duniani
💥Je niwaze nini ili niwe bora??
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Bila Shaka utakuwa unajiuliza swali hili
💥Naomba nikupeleke katika kitabu cha wafilipi 4:8
🌹8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
👉🏼Mambo nayo ndio unatakiwa kuyatafakari siku zote....kamwe hutajuta
👉🏼katika huo mstari chambua neno moja moja...lina maana kubwa Sana.
Ukiwaza hayo yatabadilisha mfumo wa kutenda na hatimaye kukujengea Imani bora na character bora zaidi
Mungu akubariki,
Mwal.Chavala PM Ezekia
Online Gospel sermons,
Ogschavala@gmail.com
+255677904755
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments