GOD ON THE SCENE

GOD ON THE SCENE(Matokeo ya Ziara ya Mungu katika maisha  yako💪🏼💪🏼)
Na Mwal.Chavala PM Ezekia.





Kuna ziara nyingi za Viongozi wa Nchi,na kila wanapofika maeneo ya ziara  kuna changamoto zilizopo maeneo Yale huwa zinatatuliwa

🔥Haiwezekani muheshimiwa Raisi akaja kutembelea katika eneo lako halafu barabara ikabakia na makorongo yake...kuna namna anapokuja Yale makorongo korongo huwa yanafukiwa(wakati huo huwezi kujua nani anafanyaga na kutoa ile order ya kufanya marekebisho..Ila utakuta tu Greda na Excavator ziko barabarani zinafanya matengenezo maana Raisi anakuja..

*🌎Unapomualika Yesu katika maisha yako,tegemea mabadiliko makubwa ambayo Hata hujawahi kuyajua*
🔥nakosa lugha ya kuelezea ,lakini kiufupi Yesu hawezi akaja kwako halafu akakuacha na matatizo yaliyokutesa miaka yote...

*🔥Soma Yeremia 33:3-----*
*3 Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.*
(Unapomuita anakuja.....kinachotokea hata mambo yaliyokuwa huyajuai Sasa utayajua)

*🌹atakuonesha Fursa mpya,Milki mpya ,Plan mpya ,na mipango mipya Yenye Tija kwako.*

*6 Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.*
*🌹Akishafika...tegemea Amani,Uponyaji na Afya😅*
*7 Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda, na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga kama kwanza.*

*🌹ahahahaa wafungwa waliofungwa ...wanapata msamaha na kurudishiwa Uhuru wao😅😅😅  anapokuja tu ...Haya yote hutokea banaaa*

*8 Nami nitawasafisha na uovu wao wote, ambao kwa huo wamenitenda dhambi; nami nitawasamehe maovu yao yote, ambayo kwayo wamenitenda dhambi, na kukosa juu yangu.*

*🌹Kutakaswa na Msamaha wa dhambi...vinatangazwa on the spot*

*9 Na mji huu utakuwa kwangu jina la furaha, na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote ya dunia, watakaosikia habari ya mema yote niwatendeayo, nao wataogopa na kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na amani nitakaoupatia mji huo.*

Na zaidi ya hayo...unapata Amani na furaha na utaishi Raha Mstarehe🤣🤣

💥Mpendwa mwanafamilia ...sijajua Kama mwenzangu ukisoma Haya maandiko huwa unaelewaje...Ila Mimi naona Nina sababu ya kumwita Mungu(Yesu) maana anapokuja eneo la tukio...mambo Haya yote hutokea pale anapofika

*#Matokeo ya ziara za Mungu katika maisha yako#*
Nikutakie siku njema

Mwal.Chavala PM Ezekia

©️Ogschavala@gmail.com
+255677904755

©️Jiunge nasi kwa kubonyeza link hii
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA

©️Download application yetu ya online gospel sermons kutoka play store upate masomo yetu ya kila siku

Nenda google play kuipata

©️Fuatilia page yetu Facebook..Gospel Sermon Ministries na Instagram..Mwal..ezekia_Chavala official.

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.