FACT MINIMISE FEARS

NGUVU YA TAARIFA SAHIHI
*the power of right information*



🌎na Mwal.Chavala PM Ezekia
Idadi kubwa ya watu ambao wanakufa kwa magonjwa ya kutisha ,sio kwa sababu Yale magonjwa yanawaua ,Ila ni kwasababu ya taarifa za hofu kuhusu Yale magonjwa ambazo zinawamaliza na hatimaye wanakufa mapema kabla hata ugonjwa haujawaua

*🌹Tafiti  zinaonesha ,wagonjwa wengi wa Presha wanakufa kila baada ya kusikia taarifa mbaya,zenye kustua,zenye majonzi na simanzi*

🌎Kwa kadri unaposikia taarifa mbaya kuna mambo yafuatayo huwa yanatokea
*1️⃣Postiponment(Kuahirisha mambo)*
🌹Kama ukisikia kuwa biashara uliyotaka kuifanya ,kuna mwenzako amefilisika juzi tu..bila Shaka utatamani kuahirisha na kushindwa kutimiza malengo yako katika biashara hiyo


*🌹Ndoto za watu wengi Sana zimekufa kwa sababu ya kuahirisha ahirisha wakiwa na hofu ya kuanza kuzitimiza...hofu hiyo inatokana na Taarifa mbaya kuhusu mambo wanayotamani kuyafanya.*

*Kuahirisha sio jambo jema....Kumbuka Kama Yesu angelisema Baba ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke akaahirisha kufanya misheni yake ya kuja kuokoa mwanadamu kitu gani kingetokea??*

➖Kuahirisha sio jambo jema hata kidogo
➖Taarifa mbaya husababisha kuahirisha ndoto yako
➖Maombi ya Yesu ya kusema kikombe kile kimuepuke hayakujibiwa kwa kuahirishwa Ila kumpatia Nguvu za kupambana na mauti pale msalabani

*Mathayo 26:39*
*39 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.*

Maombi Haya yalisababishwa na
⚖️Mateso
⚖️Kifo
⚖️Udhalilishwaji ambao Yesu akiwa na mwili wa ubinadamu asilimia 💯 na mwili wa Uungu 💯
Kuna wakati aliingiwa na uchungu...kutokana na taarifa mbalimbali zinazoeleza uchungu na Yale maumivu yaliyopo katika kuteswa na kifo cha dhihaka

*📌God Proves that postponement is not a solution to any challange*

*2️⃣Taarifa mbaya Husababisha kukimbia ,na taarifa njema husababisha kurudi kwenye himaya yako*

*Mathayo 2:19*
*19 Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri,*

*20 akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.*

21 Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli.
*🌹Ni taarifa ya Malaika iliyo njema ndiyo iliyowafanya Yusufu ,na mkewe Mariamu warudi Nyumbani kwao Israeli.*

🤔Unapokuwa umepewa taarifa mbaya huwa zinaharibu kabisa mfumo wa maisha yako

Leo nataka nikwambie ...dawa ya Hofu iliyotengenezeka ndani yako kutokana na Taariifa mbaya ni *Taarifa Njema*

🌹Badili chanzo cha taaarifa ,Kama chanzo hiki kinakutangazia habari za Mauti,kushindwa,kusalitiwa,kukosa uwezo Fulani,basi leo naomba nikuletee chanzo kipya cha taarifa kinachoweza kukueleza habari za

💪🏼Ushindi
💪🏼Matumaini
💪🏼Uzima
💪🏼Upenyo
💪🏼Nguvu
💪🏼Kibali
💪🏼Furaha
💪🏼Kufaulu

*Chanzo hicho ni NENO LA MUNGU**

3️⃣Unapoijua kweli,inaondoa hofu zote ndani yako
Yohana 8:32
*Mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru*

🌎Katika maisha yako usiruhusu Hofu itawale maisha yako
*#Badili chanzo cha taarifa#*

*#Sikiliza habari Njema#*
Mwal.Chavala PM Ezekia

Online Gospel Sermons

+255677904755
Jiunge nasi kwa mafundisho ya kila siku hapa OGS
Bonyeza link hii kujiunga
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.