NGUVU YA USHAHIDI-EVIDENCE
Hakuna kitu kinanguvu katika maisha ya binadamu Kama ushahidi ...maana
⚖️Hata Kama umehukumiwa kuuawa..Kama ukijipanga vizuri na kutengeneza ushahidi unaweza kuachiliwa huru
⚖️Mahakama zote zinahukumu kesi kulingana na ushahidi...ushahidi unapokamilika ndiyo ambao unatoa matokeo na hukumu ya kesi zote
⚖️Tuna amini kuwa Kweli Yesu ni Mungu kwa sababu ya ushahidi wa kazi zake anazozifanya katika maisha yetu
⚖️Tunashinda hofu ya kila namna kwa sababu ya ushahidi unaofukia taarifa mbaya ...lakini pia watu wanapatwa na hofu kutokana na ushahidi wa mambo mabaya wanavyoona yanaendelea..
🌹Ukikosa ushahidi(evidence) ni vigumu Sana kushinda kesi...lakini pia ukikosa ushahidi hata Kama haukuwa na makosa kuna uwezekano ukashindwa kesi hiyohiyo
Sasa ushahidi ni nini?
Ushahidi ni taarifa zinazoelezea ukweli kuhusu tukio lililopo na namna lilivotukia..
Ujanja ni kuwa na taarifa sahihi....baada ya hapo Umeshinda
Katika mathayo 4:1-11ukisoma maandiko Haya utaona jinsi ambavyo
Ushahidi wa Neno la Mungu aliokuwa nao Yesu..ulimsaidia kushinda kila kishawishi(shinikizo la shetani)
1 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.
3 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.
4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,
6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
11 Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.
Key points!
➖➖➖➖➖
1️⃣Ni rahisi Sana kushindwa vita yako hata Kama ni ndogo Kama usipokuwa na Neno la ushuhuda..
Katika ufunuo anasema Wakamshinda kwa Neno la Ushuhuda!
2️⃣Unapokuwa na ushahidi(evidence) sio rahisi kuamini uongo kuwa ...hauwezi,..kuwa wewe ni dhaifu...kuwa wewe hutafanikiwa....nk.
Maana Evidence (ushahidi) utakuonesha ukweli kuhusu maisha yako
3️⃣Hata Kama shetani atakudhihaki kiasi gani...na hata Kama Maadui zako watakuinukia kwa nguvu kiasi gani...kitu pekee kitakachowafanya washindwe mbele yako...ni pale utakapowafunuliwa kweli ya Neno la Mungu (ushahidi) unaosema wewe ni Mshindi💪🏼💪🏼💪🏼
🌹Naongea na Mtu mwenye
⭕Hofu ya kuthubutu
⭕Hofu ya kifo
⭕Hofu ya kushindwa
⭕Asiyejiamini katika mambo yake
⭕Asiye na matumaini
Tafuta ushahidi...evidence...kisha kata rufaa...kesi yako utashinda tena mchana kweupe
Mwal.Chavala PM Ezekia
Online Gospel Sermons
Ogschavala@gmail.com
+255677904755
Join us today!
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments