CREDENTIALS-NGAZI ZA MAAMUZI


- CREDENTIALS(NGAZI ZA KIMAAMUZI)

Credentials ni sifa au ngazi fulani ambayo inampatia mtu kuweza kufanya maamuzi kwa kiwango fulani

💥Ingekuwa katika Jeshi ..ningesema Idadi ya nyota ulizonazo  .zinazokutambulisha Ranki yako ya ukubwa  katika Jeshi

💥Ukubwa wa Rank uliyoko ndiyo inayoamua akina nani wawe chini yako na wakupigie saluti

🔥Katika Ulimwengu wa Roho ..kuna kitu kinaitwa Spiritual Credentials,yaani NGUVU YAKO YA KIMAAMUZI katika ulimwengu wa Roho

💥Ni kweli wote mnaweza kuwa wa Kristo wazuri,lakini kuna mtu anauwezo wa kufanya vitu fulani ambavyo wewe huwezi kuvifanya

👉🏾sasa usishangae na kusema kwa sababu wewe huwezi kuvifanya basi haviwezekani! Mungu bado anafanya mambo makubwa sana kupitia watu wake hapa Duniani

*Leo nataka nizungumzie mambo machache yanayotofautisha* *mamlaka kati ya mtu mmoja na mwingine*



1⃣Kiwango cha Elimu sahihi ya Kimungu

Hata katika Dunia ..mtu mwenye Elimu kubwa ..yaani anayejua mambo mengi kukuzidi wewe Bila shaka ni lazima mtatofautiana tu hata mshahara,cheo chake kazini,na pia hata katika utendaji

Sasa katika Ulimwengu wa Roho,Mtu ambaye anasoma sana Neno la Mungu,automatically huwa anapewa credential(wadhifa ) mkubwa zaidi..yaani anapewa Neema ya Kufanya mambo Makubwa zaidi kuliko yule asiyekula sana Neno

Kwa lugha nyingine ningesema Ili ukue Kiroho na uwe na mamlaka kubwa katika Roho...Bugia sana NENO LA MUNGU

Biblia inasema
*NENO LA MUNGU NA LIKAE KWA WINGI NDANI YENU*

*Soma Joshua 1:8-9*

*8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.*

*9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.*

Sasa unapokuwa na Neno la Mungu kwa Wingi..credential yako ya kiutendaji ndani yako inapanuka...yaani unaongeza *NYOTA* za heshima katika Ulimwengu wa Roho

*2⃣Maombi*
Jambo la pili ambalo linaongeza credential(mamlaka katika ulimwengu wako)
Ni maombi

*Maombi ni mtambo wa kutoa Amri na kufyatua kila aina bomu la mashambulizi*

Sasa maombi yanatuwezesha ..kuonesha ule uwezo wetu wa kutoa Amri katika Ulimwengu wa Roho

Mkristo yeyote asiyeomba..nimesema katika sermon iliyopita kuwa ni sawa na Commander asiyekuwa na maamuzi

*Maamuzi yako yatadhihirishwa katika maombi unayoomba*

Sasa naomba nikuache na haya mambo mawili

*Soma pia Mathayo 7;7*(andiko ulilolisoma na kulisikia mara nyingi zaidi) ila yawezekana hukujua kuwa kwa kufanya hivyo unajiongezea credentials katika ulimwengu wa Roho

 ➖➖➖➖endelea kufwatilia masomo haya kila siku kutoka Online Gospel Sermon
+255621029725
Jiunge sasa buree! Kwa kubofya hapa

https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.