TABIA ZA UPENDO WA KWELI
TABIA ZA UPENDO WA KWELI
➖➖➖➖➖➖➖➖
1Korintho 13:4-8
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
KEY POINTS
➖➖➖➖➖
1.UPENDO HUVUMILIA
Ukiona unaweza kumvumilia mtu hata kama amekukosea,basi tambua kuwa unampenda,ila usipoweza,kufanya hivyo haumpendi mtu huyo
2.UPENDO HUFADHILI
Fadhili limetokana na na Fadhila..ni kama vile kumsaidia mtu ambaye hakuwa na msaada.
Unapofadhili(unapowasaidia wengine) ni tabia mojawapo ya upendo.
Ukiona husaidii wengine..wewe hauna Upendo na hauna Mungu ndani yako
3.UPENDO HAUHUSUDU
Husudu limetokana na neno Husuda,
Husuda ni hali ya wivu mbaya .
Ukiona unahusuda(kijicho) dhidi ya ndugu zako basi hauna upendo na wala hauna Mungu ndani yako
4.HAUJIVUNI
Ukitaka kila kitu uonekane wewe ndo mwamba..nenda kalale tu kazi imekushinda..huna upendo
5.HAUONI UCHUNGU
Huwezi kunambia kuwa unanipenda halafu unatunza mauchungu Moyoni hadi unaumwa..huo sio upendo
6.HAUKOSI KUWA NA ADABU
Unawezaje kujifanya unaupendo halafu ukakosa adabu?
7.Huvumilia,huamini,yote
Tupendane.maisha hapa Duniani ni mafupi sana.tuache unafiki
Ezekia Chavala
OGS:Dir,
ogschavala@gmail.com
+255621029725
https://chat.whatsapp.com/K3lnh9YaO7Y2Z3SA2MBudI
No comments