OGS -seminar  DAY 5
FUNGUO ZA VIWANGO VINGINE
*(KEYS TO NEXT LEVELS)*


*Ufunguo wa 4* *NNE:PARTINERSHIP(UBIA&USHIRIKISHAJI)*
🌎Mungu alipomuumba mwanadamu,hakuona ni vema awe peke yake ,akamfanyia msaidizi( Eva)
*Kwa nini??*
1️⃣Alitambua kuwa mwanadamu hawezi kufanya mambo yote peke yake,anahitaji mtu wa kumsaidia.

2️⃣Alitambua kuwa ,upweke ni kitu hatari kuliko ugonjwa
Ndiyo maana Biblia inasema *Heri wawili kuliko mmoja*

3️⃣Alitambua kuwa ili kazi ifanyike kwa ubora ,ni lazima Ifanywe na mikono ya watu zaidi ya mmoja


*Swali!*
*Yesu ni Mungu,lakini kwa nini aliwachagua wale wanafunzi 12,wakati alikuwa na uwezo wa kufanya mambo yote yeyr mwenyewe?*

*Jibu!*
*🌹Alikuwa anatufundisha kuwa ushirikishaji watu wengine katika unachokifanya ni jambo bora Sana na ni kanuni nzuri ya kukusaidia kupanda viwango vingine vya Mafanikio*(key to next level)

🌹Unadhani ni kwa nini Mungu alimuandaa Haruni asaidiane na Musa katika Kuwatoa wana wa Israeli kule Misri?

👉🏼Ni partnership(ushirikishaji wenye kuleta matokeo makubwa zaidi)

➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
1️⃣Kama jambo unalolifanya ungewatafuta (kuwashirikisha wataalamu wa hicho kitu ,ungeshafika mbali Sana,Ila unakwama kwa sababu hutaki kuwashrikisha wengine(partnership)

2️⃣Stress na mawazo uliyonayo yanayokusumbua,Kama ungempata mtu sahihi angeweza kukufanyia counselling ukapona hadi ukashangaa
Unaendelea kuumia kwa ndani kwa sababu hujashirikisha wengine walio sahihi(partnership)


3️⃣Kuna maisha yanakuwa magumu kwako kwa sababu hautaki kuthubutu kuoa au kuolewa,Ila nikwambie ukweli Kama ukimpata patiner (mke au mume sahihi) kuna vitu vitachipuka ndani yako hadi utashangaa)
*Tafuta Partner sahihi😅😅*(acha kuchelewesha watoto shule)

4️⃣Hata katika Makanisa,Kuna huduma zile tano kwa sababu ya kufaidiana (partnership) ndio maana kanisa lisipopata huduma mchanganyiko wafuasi wanakuwa na utapiamlo wa kiroho
Katika wakorintho anaeleza
➖Mitume
➖Manabii
➖wainjilisti
➖wachungaji
➖walimu(akina chavala)😅😅😅

Sasa ukiona kuna moja ya huduma zinakosekana...chunguza Sana...kuna namna afya ya washirika Kiroho huwa inateteleka


5️⃣Ukitaka kufanikiwa kwa haraka ...tafuta partners sahihi,Wewe huwezi kufanya mambo yote ,Ila unauwezo wa kufanya jambo uliloumbiwa kufanya kwa ubora zaidi,Sasa unawahitaji watu wa aina mbalimbali wakusaidie katika
➖Biashara
➖Elimu
➖Huduma nk.

🇹🇿Nb..sijakuandikia maandiko kwa sababu najua ,nimetumia mifano wazi na iliyozoeleka Sana katika Biblia...Ila Kama unashida na maandiko usisite kunitafuta inbox nitakupati..yote niliyoyatumia


😅Ifike wakati usiseme ngoja nikufungulie kitabu cha Mathayo...Ila wewe ndo uwe Kama Mathayo..yaani Neno na like kwa wingi ndani yako kiasi ambacho patiners wako (wasaidizi)marafiki zako wakikuona waseme huyu jamaa anaongea Kama Mathayo😅

Hata kusema kwake Kama Mfuasi wa Yesu👉🏼

Tukutane session ya pili
Mwal.chavala.PM Ezekia

+255677904755
Ogschavala@gmail.com
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.