TENGENEZA MAZINGIRA RAFIKI-KEY TO NEXT LEVEL
*SESSION 2B...Mchana..13-3-2020*
*TENGENEZA MAZINGIRA RAFIKI YA KUKUPATIA KIBALI*
*🌹*Boresha Wasifu wako(CV)*
Karibu tena katika muendelezo wa Funguo za viwango vingine,
🌎Mchana huu naomba nikupatie njia nyingine ya kuboresha Mazingira yako ili yawe Rafiki katika kukupandisha Viwango Vingine.
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Boresha CV yako
📌Utaungana na Mimi kuwa kila eneo unalokwenda kutafuta kazi,au sapoti ili kufanya mradi (project) kuna taarifa za wasifu wako huwa zinahitajika Sana(CV)
*🌹Unaweza ukawa na uwezo Mzuri Sana wa kufanya kazi,unajua Lugha vizuri Sana,na una kila Sababu ya kupata kibali lakini Kama CV yako haiko vizuri,jiandae kukataliwa*
👉🏼CV ni jumla ya Experience(au uzoefu) ambao mtu anaupitia na kuupata na hatimaye unakuwa sehemu ya maisha yake.
👉🏼Ule uzoefu ndio unakutengenezea mazingira ya kupata kibali maeneo Fulani Fulani
*Soma 1Samweli 17:34*
*34 Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi,*
*35 mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua.*
*36 Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.*
37 Daudi akasema, BWANA aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na BWANA atakuwa pamoja nawe.
39 Naye Daudi akajifunga upanga juu ya mavazi yake, akajaribu kwenda; maana alikuwa hajavijaribu. Daudi akamwambia Sauli, Siwezi kwenda na vitu hivi, maana sikuvijaribu. Basi Daudi akavivua.
🌹katika maandiko nayo kuna kitu nataka Nikuoneshe hapo;
*1.Hakuna Mtu ambaye angeamini kuwa Daudi angeweza kupambana na yule mfilisti ,mpaka Pale Daudi alipotoa ushuhuda wake kule Porini(cv) yake.*
2.Ushuhuda wa CV yake Ulikuwa na Nguvu kuliko Goliath..
Yaani uwe na taarifa zinazoonesha uwezo mkubwa uliowahi kuuonesha kuliko kilichopo mbele yako,
Maana kila mtu na kila Ofisini huwa wanajiandaa kwao tadhari za Misukosuko,Sasa Kama hauna Uzoefu wa Misukosuko bado utakuja kukwama Mbele
🌹CV yako Iwe kubwa kuliko unachotaka kukifanya
3.CV yeyote haishuki kutoka Mbinguni,huwa inatengenezwa 😅😅😅
🌹Kila mtu anayonafasi ya kuchagua kuwa
➖Mchapakazi
➖Asiyechagua chagua aina za kazi
➖Mwenye kuthubutu kupambana na Changamoto Kama Daudi kule Machungoni
Mtu anayefanya mambo Haya ni rahisi Sana kuweza kupata kibali maana CV zake zinaruhusu
*4.Jifunze kuinadi CV yako,bila kufanya Hivyo hakuna mtu atakaeona unafaa eneo Fulani*
Wale waisraeli wote hawakuwa wanajua kuwa Daudi aliweza kupambana na Dubu na simba...mpaka pale alipojisema mwenyewe kuwa alipambana na Dubu
🌹Dont Hide your CV and your experience yako na uzoefu wako
🌹Ukikalia nayo makaratasi hakuna siku utapata upenyo wa kuyatumia💪🏼💪🏼💪🏼
Endelea kutengeneza Mazingira ya kupenya Viwango vingine
Mchana mwema.
Mwal.Chavala.PM Ezekia
Online Gospel Sermons
Ogschavala@gmail.com
Jiunge nasi Sasa kwa kubonyeza link hii
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments