START NOW-ANZA SASA!

ANZA SASA
Watu wengi wamekuwa na mipango mingi Sana  katika maisha yao lakini tatizo sio watekelezaji


Hata uwe na mipango mizuri na yenye tija Sana Kama wewe sio mtekelezaji huwezi kufanikiwa

Kingine kinachosumbua hata wale wachache ambao wanaamua kuanza kufanya kitu ...ni kukata tamaa mapema baada ya kuona Picha waliokuwa nayo inatofautiana na like walichoweza kukifanya kwa hapo awali

Nikwambie tu mtanzania mwenzangu kuwa,huwezi siku ya kwanza ukaweza kuifanya picha iliyoko akilini kwako ..ionekane kwenye unachokifanya kwa muda mfupi hivyo...

✍️Kuna hatua za Msingi ni lazima uzipitie kabla ya kutoboa aisee
1.KUBALI KUANZA.
Hii ni hatua ambayo watu wengi wanaiogopa Sana.maana inahitaji Nguvu kubwa Sana

Katika kitabu cha mwanzo 1:1-2
Mungu aliamua kuumba Dunia (Mbingu na Nchi)
*"Hapo mwanzo Mungu aliumba Mbingu na Nchi"*

Ifike wakati na wewe useme

Hapo mwanzoni nilianza duka na mtaji wa sh laki moja tu😅😅😅😅

Hapo mwanzo nilianza huduma nikiwa sina hata pesa

Hapo mwanzo nilianza kazi nikiwa sina hata kitand a wala godoro💪🏼💪🏼

*Ukiweza Kuthubutu kuanza kuna hatua ya pili Bwana atakupeleka*

2.NGAZI YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA AWALI

Nakwambia ukweli...kitu cha kwanza utakachokutana nacho baada ya kuanza kufanya kitu flank..ni changamoto

Kama ni huduma utaina Kama vile hakuna mtu anayekusikiliza vile

Nikwambie tu ukweli...kuna wakati nilipoanza ogs..nilikuwa napost sermon yangu Facebook page yangu..halafu sioni hata mtu mmoja akiwa Ame like wala Ku comment chochote

Wakati huo hili group la ogs lilikuwa na watu watatu tu...yani Mimi,mkewangu pamoja na Jamaa mmoja anaitwa Eliya😅😅

Haikuwa kazi rahisi kuendelea na huduma hii ya ogs...lakini kadri ninavyozidi ..najua sio sawa na nilikotoka..hata Kama Sasa bado hatujafanikiwa lakini Sasa sio Kama tulivoanza

✍️Ukirudi katika kitabu cha mwanzo 1:2-3 changamoto Kubwa Mungu anakutana nayo ilikuwa *ni Giza Nene katika Dunia(nchi aliyoiumba)*

Unaona ameumba kitu cha kwanza..hata kabla hajaanza kukifaidi...anakutana na changamoto ya Giza Nene....anaamua kuanza kusolve.


3.NGAZI YA MABORESHO
Hatua ya tatu utakayoipitia katika kuanza kitu ni hatua ya maboresho

Na maboresho Mara zote huwa yanatokana na changamoto ulizokutana nazo

✍️Mungu alipoona Giza..akaamua kuweka Nuru(Haya ni maboresho makubwa)

Ogs tulianza na Sermon za kawaida..baadaye tukaingia kwenye application ya ogs...inayopatikana play store...Kama hujadownload itafute kule utaiona..

*➖sasa maboresho hayaji Kama hakuna changamoto..ndio maana Ninapenda Sana changamoto kwa sababu ..zinanisaidia kuona fursa za maboresho*


4.NGAZI YA KUPIGA HATUA KWA HARAKA
Ukishaweza kufanya maboresho ya awali...huwa yanakusaidia kupiga hatua kwa haraka zaidi


Kuanzia mstari wa 4 na kuendelea..Mungu aliposolve tatizo la Giza kwa kuleta nuru...ndio hapo uumbaji wa vitu vingine ukawa ni rahisi zaidi


🌹kuanzia pale ikawa rahisi kuumba mimea maana mwanga wa kujitengenezea chakula so upo?

🌹ikawa rahisi kuumba hata wadudu..maana wataweza kukaa na kuka matunda ya mimea inayotegemea mwanga..kutengeneza chakula💪🏼💪🏼💪

5.NGAZI YA TATHIMINI(ASSESMENT)

Baada ya hatua hizi zote ,kuna ngazi ni lazima uipitie ya kujitathimini

Mzee alikaa akaangalia akaona vyote alivyovifanya ni vyema😅😅😅😅😅

Akaendelea kumalizia malizia na uumbaji...na baadae akamfyatua mwanadamu💪🏼💪🏼💪🏼💪🏼💪🏼💪🏼

*The greatest achievement*

*6️⃣mafanikio (achievements) phase*
Ukiweza kupita ngazi zote hizi...kuna kitu cha muhimu ambacho utakifikia...yani Yale mafanikio ya kweli

🌹Mungu wetu alikuwa anatufundisha kuwa ..mvumilivu hula mbivu...ninawaza tu kwa sauti kuwa ..Kama siku ya kwanza angemuumba mwanadamu,kuna vitu yawezekana visingekuwa sawa..maana huyu mwanadamu angekuka nini..na angefanya kazi gani?

Mungu anaakili Sana alitambua kuwa Mwanadamu atakuwa ndio msimamizi wa kika alichokiumba na ndio mana akimuumba mwishoni😅😅

📌Kuna greatest achievements zitakupata usiporuka hatua za hizi ngazi za kuelekea mafanikio

Endelea kutufwatilia ogs
Mwal.Chavala PM Ezekia

+255621029725
Karibu
Online Gospel Sermons.
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.