UPENYO-BREAKTHROUGH

MATOKEO YA KUWA NA UTUKUFU WA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO
👉🏾katika vipindi vilivyopita nimezungumzia mambo au matokeo manne ya kuwa na utukufu wa Mungu
1⃣Kung'ara na kuchanua
2⃣Kubadilishwa kwa historia mbaya ya maisha yako
3⃣Kuvunjika kwa mipaka yako(Limitation)
4⃣Kupata heshima katika maisha yako


Sasa leo naenda kukufundisha tokeo la tano ambalo ni
*5⃣KUPATA UPENYO KATIKA MAISHA YAKO*
💥Upenyo ni ile hali ya kupita kiugumu ugumu  au ile hali ya kufanikiwa kupita eneo ambalo halikuwa rahisi kupita katika hali ya kawaida

👉🏾Ule uwezo wa kupita katika njia ambayo kimsingi hukuwa una sifa ya kupita

👉🏾Uwezo wa kuishi wakati huo ulitakiwa kufa

👉🏾Uwezo wa kuwa na kazi wakati haukutakiwa kuwa nayo

💥Ni ile Neema ya Mungu inayokuwa juu yako na kukusaidia kuyafikia malengo fulani..wakati kila mtu wa ngazi au rika lako ameshindwa(breakthrough)

✍🏼sasa Ni neema ya Mungu na utukufu wa Mungu pekee vikikufunika unao uwezo wa kuingia katika ngazi hizi

*Soma 2falme7:3---*
*3 Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe?*

*4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu.*

*5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu.*

*6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.*

*7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao.*

*8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha.*

*9 Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme.*
.katika maandiko haya tuliyoyasoma,kuna vitu vya msingi naomba nikuoneshe hapa


1⃣Wale wakoma walikuwa hawana njia nyingine ya kupona..ilikuwa wasubiri kufa tu maana njaa ilikuwa kubwa sana..mjini...


2⃣walipoamua kuanza kuwaendea washami,utukufu wa Mungu uliwafunika ndipo

*Kishindo cha Miguu yao kikawatisha wale washami wakaacha kambi zao na kukimbia💪🏼💪🏼💪🏼*

3⃣Kumbuka hawa jamaa walikuwa wameliwa na ukoma...sio rahisi kwa mtu mwenye ukoma miguuni kuwa na kishindo kikubwa katika kutembea😅😅

Mara nyingi hata namna ya utembeaji wake ni ule wa kuchechemea au kunyata nyata


💥Lakini ...pamoja na mwendo wao wa kidhaifu...Utukufu wa Mungu uliwafanya washami kukimbia mbele yao


🔥Nataka nikwambie siku ya leo

Yawezekana ni kweli hauna sifa za kuingia eneo fulani,yani wewe ni sawa na wale wakoma,

*Lakini Utukufu wa Mungu unapokuwa juu yako...hakuna adui atasimama mbele yako kukuzuia usipenye*


Utapenya na kutoboa ..katika Jina la Yesu

*Ukisoma Rumi 8:31*
*31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?*
32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?

Mungu akiwa upande wetu ana maana kuwa...Utukufu wa Mungu unapokuwa pamoja na sisi..adui gani wa kusimama kinyume chetu???

Nikutakie mpenyo mkubwa katika kila jambo lako siku ya leo

💥Mwal.Chavala Pm Ezekia
Online Gospel Sermons

Ogschavala@gmail.com

Kujiunga na Online Gospel sermon bonyeza link hii bure

https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA


No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.