KEYS TO NEXT LEVELS-FUNGUO ZA VIWANGO VINGINE
*FUNGUO YA KWANZA*
CONNECTIONS( NETWORK)
Watu wengi wamekuwa wanashindwa kutoboa viwango vingine katika mambo wanayoyafanya kwa sababu wamekosa Network(connection)
🌎Mungu zamani alikuwa anashuka mwenyewe,au anatuma Kunguru kuleta chakula kwa watumishi wake waliokuwa na njaa,aliweza kutumia viumbe hata visivyokuwa hai kibinadamu ili kuwasaidia watu wake ,lakini Sasa Mungu anajibu maombi yako kwa kutumia *Connections* na Network ,
🌹Naomba nieleweke wazi hapa kuwa,haimaanishi kuwa Mungu hawezi kukupandisha Viwango kwa miujiza
➖Mungu wetu anaweza mambo yote,Ila huu ni ufunguo ambao Kama ukiutumia ni rahisi kufanikiwa bila kumsumbua sumbua Mungu atende muujiza
*🌹Maana mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru*
*➖Connection..ni ule mtandao wa watu unaowajua na usiowajua,ambao Mungu anaruhusu upite mikononi mwao au wapite mikononi mwako kwa wakati Fulani.*
✍️Mungu anaporuhusu muweze kufahamiana na mtu Fulani,huwa Ana kusudi maalumu kabisa Huwa anakuwa anatengeneza mahusiano( connection ) Kati yenu ambayo itakuja kuwasaidia kuvushana viwango vingine mbele ya safari
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
🌎Kama kuna mjuzi wa Biashara ,basi Mungu ni namba moja,maana anajua kuwa kila biashara huwa inaanza kwa mtaji mkubwa,tena wa kutoka kwa muwekezaji mwenyewe ,halafu baadae inaanza kujiendesha yenyewe
*Sasa Kama ni mtaji wa moja kwa moja wa kukuinua na kukusaidia ,Mungu alishaufanya,Sasa anatamani wanadamu mfanikiwe kwa kujiendesha wenyewe*
Na njia aliyotusaidia tuitumie ni *Connections*
*MIFANO YA BIBLIA*
1️⃣Unamkumbuka Mnnyweshaji pamoja na Yusufu,kule Gerezani wakati ule Yusufu ametupwa Gerezani?
🌹hawa jamaa walianza kufahamiana na kutengeneza connections,kwa Yusufu kumsaidia kutafsiri ndoto yake,
🌹Matokeo ya hii connection ,inakuja kumtoa Yusufu katika Gereza ,maana yule jamaa alipoona fursa ya kufasiri ndoto pale kwa mfalme..alikumbuka connection ya rafiki yake aliyeitengeneza nae akiwa na yeye Gerezani
📌Naomba niongeze sauti..kuna mtu bado hajaelewa hapa
*✍️Mahusiano Mazuri aliyoyatengeneza Yusufu kwa Yule muokaji wa mikate kule Gerezani wakiwa wamefungwa pamoja...Yale mahusiano yalikuja kumtengenezea chance Yusufu ya kutafsiri ndoto ya mfalme na kutolewa nje ya Gereza*
Matokeo yake anapandishwa Viwango vingine na kuwa Waziri mkuu...tuseme kwa sasa💪🏼💪🏼💪🏼
MUHIMU SANA
➖➖➖➖➖
Idadi ya watu unaohusiana nao katika kazi,
🌹huduma
,🌹maisha,
🌹masomo,
🌹ugonjwa,(hospitalini)) na kwingine kokote hata 🌹safarini
*,jitahidi kuitunza na kuilea maana Mungu huwa anatumia Connection(Network uliyojitengenezea awali) katika kukupandishia viwango vingine*
*Soma Mwanzo:40*
,*utapata stori nzima ya namna Yusufu alivotengeneza Network na Mnyweshaji...akiwa gerezani..na hatimaye mnyweshaji anakuja kumkumbuka mbele ya siku
2️⃣MFANO WA MWANAMKE KAHABA(RAHABU)
Katika kitabu cha Yoshua 2,:2...
Yoshua anawatuma wapelelezi waende kuupeleleza mji wa Yeriko
Huyu kahaba anaamua kujitengenezea Network ya watu hao anawaficha hali akijua anahatarisha maisha yake pia
✍️Matokeo yake,anapata kibali cha kuingizwa katika Ukoo wa Yesu Kristo😅😅
📌Kutoka kuitwa Malaya ,hadi kupenya na kuingia katia Kitabu cha ukoo wa Yesu,sio jambo dogo Kama unavodhani
📌haya yote ni matokeo ya Mtandao( mahusiano mazuri) network nzuri ya kuishi vizuri na watu
*Hebu tusome hapa...Yoshua 2:2...... kwa faida ya akina Tomaso😟*
1 Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.
2 Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili kuipeleleza nchi.
3 Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili kuipeleleza nchi.
4 Yule mwanamke akawatwaa wale watu wawili, akawaficha, akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka;
5 ikawa kama wakati wa kufungwa lango la mji, kulipokuwa giza, watu wale wakatoka, wala sijui walikokwenda; wafuateni upesi, maana mtawapata
.
6 Lakini yeye alikuwa amewapandisha darini, akawaficha kwa mabua ya kitani, aliyokuwa ameyatandika juu ya dari.
*🌹8 Tena kabla hawajalala akawaendea juu darini,*
*9 akawaambia wale wanaume, Mimi najua ya kuwa BWANA amewapa ninyi nchi hii, na ya kuwa hofu imetuangukia mbele yenu, na ya kuwa wenyeji wote wa nchi wanayeyuka mbele yenu.*
10 Maana tumesikia jinsi BWANA alivyoyakausha maji ya bahari ya Shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo mliyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa huko ng’ambo ya Yordani, yaani, Sihoni na Ogu, mliowaangamiza kabisa.
*🌹12 Basi sasa, nawasihi, niapieni kwa BWANA, kwa kuwa nimewatendea ihisani, ya kwamba ninyi nanyi mtaitendea ihisani nyumba ya baba yangu; tena nipeni alama ya uaminifu;*
13 ya kwamba mtawaponya hai baba yangu na mama yangu, na ndugu zangu wanaume na wanawake, na vitu vyote walivyo navyo, na kutuokoa roho zetu na kufa.
*🌹14 Wale wanaume wakamwambia, Uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa ihisani na uaminifu.*
15 Ndipo akawashusha kwa kamba dirishani, maana nyumba yake ilikuwa katika ukuta wa mji; naye alikaa ukutani.
Unaweza ukaona namna ambavyo huyu Rahabu anatengeneza Network...ili badaye ije kumsaidia😅
➖Kuna mambo Mengi yaliendelea hapa katikati,vizazi vikapita,lakini...kwa hakika na Rahabu amekuja kuonekana katika kitabu cha ukoo wa Yesu💪🏼💪🏼
Power of Network and connections!
Soma Mathayo 1:3-6
1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;
3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;
4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;
*🌹5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;*
6 Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria;
7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;
8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;
Nikusihi leo katika siku hii ya kwanza
➖Tengeneza Network kadri uwezavyo,itakutoa siku moja kukupandisha viwango vingine
➖Usimdharau mtu yeyote utakaekutana nae katika maisha yako,hujui lini atakuwa nani na atakuunganisha ufanikiwe wapi
➖Kila mtu anaepita mikononi mwako au unaepita mikononi make ni Rasilimali muhimu Sana ,tengeneza connection kwa kadri uwezavyo itakusaidia Sana
Nikutakie semina njema
Mwal.Chavala PM Ezekia
+255621029725
Ogschavala@gmail.com
*Online Gospel Sermon..March Seminar*
Jiunge na Darasa letu upate Neno kila siku
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments