MAENEO YA UTAWALA
Leo nikiwa nimepumzika usiku ,katika njozi kuna somo nikaanza kufundishwa,nilihisi ni ndoto ya kawaida..ila baada ya kuamka nikakuta hili somo linajirudia rudia sana kichwani...ndipo nikapata amani ya kuliandika hapa
💥Nina imani kuna mtu litaenda kumtoa mahali alipo
➖➖➖➖➖➖➖➖
Eneo kubwa ambalo linaonesha au kudhihirisha kuwa mtu ana mamlaka na nguvu ni kwenye *MLANGO*
✍🏼Mtu ukitaka umnyime uhuru ..wewe mnyang'anye funguo za mlango wake
✍🏼Ukitaka ashindwe kuwa na jeuri ..wewe mfungie ndani
Na ndiyo maana kuna magereza..ya kufungia watu ndani kwa sababu Kumfunga mtu anakosa uwezo na mamlaka yake inaishia pale
✍🏼Hata Lucifeli yule shetani mwenyewe anajua kuwa ..ili akutese vizuri ni lazima akufunge viwango vya ufahamu kuhusu uhuru wako maana ndiyo injini ya uwezo wako
Sasa MUNGU WETU ALIYE HAI
*Ana tawala Mbinguni,Duniani,Pamoja na kuzimu*
Yaani ana mamlaka katika maeneo haya yote matatu
*Sababu*
1⃣Yeye pekee ndiye mwenye funguo za Uzima na mauti
2⃣Yeye pekee anao uwezo wa kukutetea wewe na mauti hata Milango ya kuzimu isiweze kukushinda
*Mathayo 16:18*
*18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.*
.👉🏾this means...kuna namna anauwezo dhidi ya milango ya kuzimu
Namaanisha
💧Mauti
💧Dhambi
💧Kifo
💧Magonjwa ya kufisha ( Deadly Diseases) na kila aina ya Hali zinazohusiana na kuzimu
3⃣Yeye baada ya kutuokoa ametupatia uwezo wa kutawala pamoja na yeye
Yaani funguo za kufunga au kufungua
*Mathayo 16:19*
*19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.*..
Mtu aliyepewa funguo..tunategemea awe muhusika wa kufunga na kufungua mambo mbalimbali yanayomsumbua katika himaya yake
*UNAKWAMA WAPI??*
1⃣Umepewa Funguo..Jina la Yesu la kutumia kufunga na kufungua kila kitu kinachokusumbua lakini haulitumii na wewe unabaki kuhangaika
2⃣Umepewa Mamlaka ya Kukanyaga nyoka na nge (yaani mamlaka dhidi ya adui zako wote lakini bado wanakutesa mwenyewe kwanini?)
Nakushauri siku ya leo
Anza kutumia mamlaka uliyopewa kufunga kila aina ya mateso ambayo yamekuwa yakikusumbua
💪🏼Nguvu tunazo
💪🏼Mamlaka tunayo
💪🏼Uwezo tunao
Kwa hakika tutamshinda kwa Jina la Yesu🔥🔥
Hebu kuwa na wakati mzuri wa kufikiri kuhusu maisha yako na namna ulivyokuwa mateka katika ulimwengu wa Roho..na namna unavoteswa wakati huo Bwana amekupatia mamlaka ya kutiisha kila kitu mbele yako
🤔🤔Tafakari...Chukua hatua wewe ni mtawala
Mwanzo 1;27..
*26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.*
*Nakutakia utawala mwema kuanzia sasa*
Gain your Authority in Jesus name🔥🔥
Mwal Chavala Pm Ezekia
Online Gospel Sermons
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments