HESHIMA -MATOKEO YA KUTEMBEA NA UTUKUFU WA MUNGU
Katika vipindi vilivyopita ,nimezungumzia matokeo matatu ambayo ni
1⃣Kung'ara na kuchanua sana
2⃣Kubadilishwa kwa historia yako
3⃣Kuvunjwa kwa mipaka yako( limitations)
Sasa leo naomba nizungumze tokeo la Nne ambalo ni;
4⃣KUPATA HESHIMA KATIKA JAMII YAKO
💥Biblia inasema..mtu akinitumikia Baba atamheshimu
*Yohana 12:16*
*26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu*
Unapokuwa na Mungu,popote utukufu wake utakapokuwepo .ndipo na wewe utakuwepo pale na sasa utaanza kupata heshima sio kwa sababu unastahili hapana...ila kwa sababu ya ule utukufu wa Mungu unaotembea nao
*Unakumbuka wana wa Israeli waliongozwa na Nguzo ya moto usiku? kule jangwani?*
*Ushuhuda*
Musa alikuwa mtu wa kawaida sana...ila utukufu wa Mungu ulipomfunika...akapata ile hali ya utiisho wa Kimungu ndio sababu akina Kola ..na wale wana wa israeli wakorofi korofi walimheshimu na kumsikikiza
🤔🤔
Najaribu kuwaza ..kama Musa asingekuwa anatembea na utukufu wa Mungu,nani katika lile kundi angemsikikiza???
💥Najaribu kumuwaza Elisha mtumishi wa Mungu ..kwa amri yake ya kumwambia kamanda wa Jeshi Nahamani..Aende akajioshe mto yolodani mara saba..kumbuka hata hakutoka kumuona uso kwa uso..yani niseme ni kama kwa dharau vile ..kamwambia mtumishi wake ..Boazi..Hebu mwambie huyo jamaa akajichovye mto Yolodani mara sana💪🏼💪🏼💪🏼
Kama sio utukufu wa Mungu uliomfunika bila shaka asingepata ile mamlaka ya kuheshimiwa na kusikilizwa😅😅
➖Tena yawezekana ingekuwa ndo siku yake ya kukatwa kichwa mchana kweupe we unawajua wanajeshi au unawasikia??😃😃
Ila Utukufu wa Mungu ukikufunika unapata heshima
✍🏼Dawa ya watumishi wenzio wasio kusikikiza ni kuutafuta utisho( utukufu wa Mungu)
Hakuna atakaekusumbua aiseee😅😅
✍🏼Mumeo amekuwa msumbufu- wewe komaa na utukufu wa Mungu...atajawa na hofu ghafla..utadhani kuna polisi kamnyoosha ..kumbe ni ule utisho wa Kimungu ulioubeba katika maisha yako
✍🏼Washirikina wanakusumbua sumbua..dawa yao ni utukufu wa Mungu ukuvae😅😅
Wanaweza kuja kukuomba msamaha wakidhani unajua wanayoyafanyaga gizani kumbe wala hauna habari
*Sasa kwa dakika chache naomba nikupitishe kwenye sifa za mtu anayeheshimiwa!!*
💥Unajua unaweza kuwa hauoni umuhimu wa heshima ninayoifundisha hapa kama matokeo ya kufunikwa na utukufu wa Mungu,ila kwa sababu hujui haswa mtu anayeheshimiwa huwa anakuaje??
1⃣Ndugu,muheshimiwa yeyote kwanza huwa ana vyanzo vya kwake vya uchumi aisee..
2⃣huwa anatokea kwake( hajapanga ) na kama amepanga basi ni jumba la uhakika
3⃣Huwa anakuwa na usafiri wa uhakika
4⃣Bila kusahau walinzi private
5⃣Huwa halii lii njaa ,maana vyakula vipo
Unaweza kuongezea mengine mengi ambayo ni sifa za waheshimiwa
💪🏼💪🏼sasa kama haya ni ya hapa Duniani...je Baba yetu akituheshimu sio zaidi ya haya?
Ukiheshimiwa na Baba..yetu wa Mbinguni tegemea haya kwako chalii yangu!!
➖Promition zitakuwa za kwako .yani itakuwa ni kitu cha kawaida sana kwako.
➖Ulinzi wa Mungu utakuwa juu yako
➖Amani ya Mungu itakufunika
➖Uzima utakuwa ni sehemu ya maisha yako
Na mengine kibao
👉🏾aisee..tafuta sana kujawa na utukufu wa Mungu..maana kuna vitu utavipata hadi hutaamini...ila ndo vitakuwa sehemu ya maisha yako
*Ni mimi Mwal.Chavala PM Ezekia*
Wa Online Gospel Sermons
Call us
+255621029725
Tuandikie ..maoni..ogschavala@gmail.com
➖Download app mpya ya Online gospel sermons upate masomo bure..
➖fuata na u like page yetu ya facebook..
Iitwayo *Gospel sermon Ministries*
Kama hujajiunga na OGS group,bonyeza link hii hapa
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments