STRESS MANAGEMENT
MAMBO YA KUFANYA ILI KUEPUKANA NA STRESS
(STRESS MANAGEMENT)
Stress zinasababisha maumivu makali sana moyoni,na stress zinaweza kukufanya ukashindwa kuwa na furaha na Amani katika maisha yako.
Mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia kuondokana na stress
1.ZUNGUMZA WALAU MANENO ELF SITA KWA SIKU(scientifically proved)
Kwa siku ili uweze kupunguza sumu katika mwili wako,unashauriwa kuongea maneno elf sifa(6000)
Inasemekana kuwa wanawake kwa siku huwa wanaongea maneno takribani 24000 ,hii ndiyo sababu wanawake wengi ni wepesi wa kuachilia mambo kuliko wanaume
Sasa kwa kadri unapoongea sana,unapunguza kiwango cha stress katika maisha yako
2.FANYA MAZOEZI YA MWILI
Mazoezi ya mwili husaidia kupunguza stress maana mazoezi hutengeneza concentration mpya kabisa katika akili zako
Hii ni kwabsababu mazoezi husababisha kusambaa kwa damu katika viungo vyote vya mwili pamoja na ubongo,ile damu inabeba Oxygen gas ambayo ni safi..inajenga deli mpya za ubongo ambazo bado hazijashambuliwa kitaalamu.
Mazoezi yana kazi kubwa sana katika kukuondolea stress ndani yako.
3.FANYA HOBBY ZAKO
Hobby ni vitu vile unavovipendelea zaidi katika maisha yako
Inaweza kuwa ni kupiga piano,gitaa.kusoma vitabu,kuangalia videos nk
Hobby inakufanya kuacha kuwaza kinachokusumbua na kuanza kuwaza mambo Mengine kabisa.
4.LIA MACHOZI YAKUTOKE
Utagundua kuwa sisi waafrika tumekuwa na utamaduni mbaya sana...mtu
Akifiwa na mkewake ..kuna wakati mwingine tunamshauri na kunyamazisha asilie kumbe tunazidi kumtengenezea sumu Kali mwilini
Machozi huondoka na sumu za stress,kitaalamu unashauriwa kuwa na muda mzuri wa Julia ili kupunguza sumu mwilini
Wanafaida sana watu wanaopata muda wa kuomba..maana unapoomba kuna mambo mawili unayafanya kwa wakati mmoja
Moja unapeleka haja zako na unawasiliana na Mungu
Pili unapunguza sumu za stress na ndio maana jamii ya wakristo waombaji wazuri kiwango cha hofu na stress katika maisha yao huwa ni kidogo sana
5.PIGA MAYOWE AU IMBA KWA SAUTI
Zile kelele za Aisha unapoimba au unapopiga mayowe husaidia sana kukutoa katika msongo wa mawazo..
Unapofanya hivi inakusaidia kurejesha afya ya mwili wako
6.JICHANGANYE KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII
Mfano..harusi,misiba,nk
Unapienda kwenye hizi shughuli itakusaidia kusahau mawazo yanayokusumbua kwa muda mrefu.
Hata hivyo,kukaa ndani Kama utumbo,unazidi kutengeneza sumu mwilini
7.SOMA SANA NENO LA MUNGU
Wale wasomaji wa Biblia na vitabu vyenye Pumzi za Mungu watakuwa ni mashahidi katika Haya niyasemayo
Unaposoma Neno la Mungu kuna vitu lazima Roho wa Bwana ataanza kukusemesha tu na hatimaye utajikuta unapata tumaini jipya
Jijengee tabia ya kusoma Neno la Mungu na kulitafakari usiku na mchana Kama anavyoeleza katika kitabu cha kutoka 1:8
8.TENGA MUDA WA KUTAFAKARI BINAFSI.
Unapokuwa na muda wa kutafakari ni lazima ubongo wako unaondoa sumu za awali za mawazo na kukuletea mawazo mapya
Ukisoma Filipi 4:8
Hapa anaeleza aina nzuri za mawazo ambayo unatakiwa kuyatafakari
Tafakari yaliyo mema...utaepukana na msingi wa mawazo
Endelea kutufwatilia...like Facebook page yetu
Gospel Sermon Ministries
Mwal.Chavala PM Ezekia
+255677904755(whatsap)
Karibu pia kwa counselling na ushauri ...
Mungu akubariki sana.
No comments