NGUVU YA KUANZA-ACTIVATION ENERGY
Muda mchache uliopita nimepata nafasi ya kuzungumza na Mlezi wangu Brother Simbeye SD.
Kuna neno moja ameniambia ..katika mazungumzo yetu limegonga katika akili yangu likazaa hi I sermon
💥Amenambia kuna kitu mtu anacho tu Ila kinaweza kisionekane hadi pale anapokianzisha( activate)
Sasa kila kitu unachoweza kukiwaza na kukifikiri katika akili yako ni tayari kipo tu,ishu iko kwenye namna ya kukifanya kiwe hai( kiwe active) kuweza kuleta matokeo Fulani
✍️Unapoingia katika ufalme wa Mungu,kila kitu utakikuta pale,shida ni je unao uwezo wa kukimiliki?
🔥Kuna vitu vichache nataka nikupitishe halafu utaelewa vizuri kitu gani Roho wa Bwana anataka tujifunze hapa
1️⃣Adamu na Eva waliingizwa katika Bustani yenye kila kitu,na wakaishi vizuri na kupata kila kitu,hapakuwa na
⚠️Kifo
⛔Njaa
❗Magonjwa wala huzuni
*Lakini bado baada ya muda walijikuta wamefukuzwa na wakashindwa kuendelea kuvipata vile vitu bure*
( waligusa kitu ambacho ni mwiko kwao kugusa) kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya
*Mwanzo 3:24*
*24 Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.*
💔Haya yote wanayapata hawa ndugu kwa sababu tu ya kugusa kitu ambacho waliambiwa wasiguse
*✍️Fuata maelekezo unapokuwa katika ufalme,usiguse kitu ulichokatazwa matokeo yake huwa ni mabaya zaidi ya vile ambavyo unafikiria.*
2️⃣Baada tu ya Kula lile tunda la katikati Biblia inasema hapo ndipo kifo kikaanza Rasmi
*🔈Inamaana kuwa ,kifo kilikuwepo muda wote, Ila kilikuwa hakina Nguvu( Dommant) na kilikuwa kinasubiri*
*Activation Energy* kutoka kwa mtu yeyote pale ,kwa bahati mbaya Kati ya Adamu na Eva,Eva ndiye aliyepitiwa na nyoka kufanya hili tukio la Ku activate Kifo
*Message*
⭕Unao uwezo wa kuamua nini ukianzishe ( uactivate) katika maisha yako
⭕Mungu ametupatia sisi wanadamu uwezo (Funguo ) za kuanzisha( Ku activate) mambo mbalimbali
Yaani Mauti au Uzima funguo zake tuko nazo sisi hapa
⭕Chochote utakacho activate Duniani, na katika ulimwengu wa Roho kitakuwa activated na chochote ambacho hauta activate Duniani na katika Ulimwengu wa Roho hakitakuwa active kabisa
3️⃣Mwanadamu amepewa madaraka makubwa Sana katika ulimwengu wa Roho..tatizo yeye hayatumii madaraka yake
Soma
*Ufunuo 5;10*
*10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.*
Asubuhi ya Leo tulikuwa na hii mada, Ila ilikuwa kwa sura nyingine,sasa muda huu inakuja Kama
*NGUVU YA UTAWALA V/S ACTIVATION ENERGY*
Naona vile utanyanyuka kwa hasira kuanza kufanya activation ya kila kitu ambacho kilitakiwa kuwa hai, sasa lakini kimekufa
♨️Activate it in Jesus name
♨️Na kila kilicho kibaya ..usiguse button ya kuactivate ( kwa lugha nyingine wanasema usichomoe betri😅😅) achana nacho kitakusababishia kifo bure
Mwal.Chavala Pm Ezekia
Online Gospel Sermons
+255621029725/+255677904755
Kwa Maoni na Maswali
Ogschavala@gmail.com.
Kujiunga na Group la Mafundisho haya
Ogs link
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments