VUNJA MIPAKA YAKO-BREAK YOUR LIMITATIONS
Na
MWAL.CHAVALA PM EZEKIA.
Utangulizi.
Mipaka ni moja kati ya vitu vya muhimu sana maana inatusaidia
kujua tunaishia wapi,na vinakupatia nidhamu ya kujua mwisho wa uhuru wako.
Lakini kitu
kibaya sana kuhusu mipaka hasa katika ulimwengu wa kujiongeza uwezo wako,nguvu
zako,na thamani yako katika kile unachokifanya mipaka huwa inatudidimiza sana
na wakati mwingine inatufanya tubaki eneo moja kwa muda mrefu sana.
Katika makala hii nataka nikueleze njia /kanuni/mbinu za kuweza
kuivunja mipaka ya pale ulipoishia ili uweze kupiga hatua mbele zaidi ya mipaka
yako[limitations]
Sasa kabla hatujaanza kuziangalia hizo mbinu nataka
nikuweke sawa katika eneo lako la bahati na sibu!
Mtu yeyote anao uwezo wa kufanikiwa zaidi ya mipaka yake.hakuna
aliyezaliwa akiwa tayari ana mafanikio na hakuna aliyezaliwa akiwa masikini
Muhubiri 9;11d
‘‘………………Lakini wakati na bahati huwapata wote’’
Sasa katika hili nataka nikutoe
katika ile tafsiri inayokusumbua na kukuona ujione kuwa hauwezi kufanya kitu
Fulani.
Hata kama umezaliwa katika
mazingira magumu kiasi gani ,bado unayo nafasi ya kufanya mambo makubwa na
kuvunja mipaka yako .
KANUNI ZA
KUVUNJA MIPAKA
1.KANUNI YA KWANZA
TENGENEZA
FURSA ZA KWAKO
Kuna kitu kinachokutofautisha wewe
,mimi pamoja na Yule
Kitu hicho huwa ni zile fursa
tunazozipata na kuzitumia.kwa kawaida fursa huvutia neema.
‘Mariamu aliweza kupitishiwa kumzaa
Yesu kwa sababu alikuwa amejitengenezea Fursa’
Fursa ya Mariamu ilikuwa ni KUWA BIKIRA
yaani kujitunza
Mathayo 1;23
‘Tazama bikira
atachukua mimba naye atazaa mwana,nao watamwita jina lake YESU,[Emmanueli]’
Sitaki tugombane na watu hapa,ila
natamani nikuoneshe kuwa fursa unazoweza kujitengenezea ,zinauwezo wa kubadili
kabisa historia ya maisha yako.kuna fursa ambayo Mariamu aliitengeneza yeye
mwenyewe ila matokeo yake ikaja kuvunja mipaka yake akawa mama wa Yesu
Tafuta BIKIRA YAKO eneo ambalo halijaguswa na mtu anza kufanyia kazi
,utaona mafanikio makubwa,usitumie vitu vya watu tu,buni vya kwako pia.
·
Biashara wasiyoifanya wengi
·
Mazingira wasiyoyapita wengi
·
Ubunifu usiogundulika kwa wengi
Haya ni baadhi ya maeneo yenye
ubikira ambayo yanauwezekano mkubwa wa kukufanya uvunje mipaka yako!
2.KANUNI YA PILI
KULA TAARIFA SAHIHI[CHAKULA SAHIHI]
‘‘UNACHOKULA NDICHO
KINACHOKUTENGENEZA VILE ULIVYO’’
[kula taarifa sahihi].
Bila shaka wote tunajua matokeo ya
kuwa kibonge ni kwa sababu unakula aina Fulani ya vyakula na kama sio hivyo
basi umerithi kutokana na genes[vinasaba] vya wazazi wako
Sasa aina ya taarifa
zinazokuzunguka ,kama zinaelezea kushindwa shindwa tu ndugu yangu muda sio
mrefu utajikuta na wewe umekuwa mshindwaji wa kila kitu
Na kama utazungukwa na taarifa
zenye ushindi ushindi na watu watakaokuzunguka watakuwa wenye akili zenye
mitazamo chanya ,wala haitakuchukua muda kuweza kuvunja mipaka yako
Hata taarifa unazozisoma pia
zinazokuingia zina mchango mkubwa sana katika kukufanya vile ulivyo leo
Hivyo ulivyo leo ni matokeo tu ya
taarifa ulizonazo kichwani kwako
Ningekushauri sana jitengenezee jamii ya watu wenye mtazamo chanya kuhusu
maisha maana watakulisha taarifa chanya zitakazosababisha uweze kuvunja mipaka
yako.
‘‘Mithali 18;21’’
‘‘Kimtokacho mtu ndicho kilichoujaza moyo wake’’
3.KANUNI YA TATU
BORESHA HUDUMA YAKO.
Naomba nikupatie mfano huu
Siku moja nilikuwa natafuta suti
kwaajili ya kuvaa siku ya harusi yangu
Nilizunguka sana katika maduka
mbalimbali ya POSTA pamoja na Kinodoni,cha kushangaza kila Duka nililopita suti
zilikuwa nzuri sana ila tatizo ilikuwa ni bei kubwa sana ,suti iliuzwa laki
tano,laki nne na nusu na kuendelea….
Baada ya muda nikaamua niangalie na
Kariakoo pale ,nikaikuta moja tena yenye nembo moja na ile ya Kindondoni na
Posta ,na hata size ilikuwa ni moja lakini hapa Kariakoo ilikuwa inauzwa
shilingi laki moja na elfu hamsini
Nilichogundua ,ubora wa huduma na
mazingira ambayo suti zile ziliwekwa na kupangwa ndio ambao ulivunja mipaka ya
bei za kawaida za zile suti
Sasa kila kitu unachokifanya kama
ukiboresha mazingira ya ufanyaji ni lazima kitakufanya uvunje mipaka yako
Hata bidhaa ina uwezo wa kukulipa
zaidi ya vile ulivyotegemea kama utaitengenezea mazingira bora
Hujawahi kusikia waswahili wanasema
‘‘CHEMA CHAJIUZA NA KIBAYA CHA JITEMBEZA?’’
·
Shida siyo
biashara unayoifanya ,shida ni je umeiboresha kwa kiwango gani?
·
Shida siyo
kazi yako,ila shida ni je unaipenda na kuitengenezea mazingira ya kuwavutia
wateja kwa kiwango gani?
JEUKIFANYA VEMA HAUTAPATA
KIBALI????????
KWA LUGHA NYINYINE
JE UKIFANYA KWA UBORA
HAUVUNJA MIPAKA YAKO??????
Kuna uhusiano mkubwa sana
kati ya kufanya vema na kupata kibali au kuvunja mipaka yako
MWANZO 4;7a
Kufanya vyema lazima utapata kibali tu .
4.KANUNI YA NNE
GUSA MAISHA YA WATU
Naomba nikuhakikishie kwa asilimia zote 100,ukitaka kuvunja
mipaka yako yoyote ile ,fanya kitu ambacho kitagusa maisha ya watu moja kwa
moja
·
Utavunja
mipaka ya umri wako wa kuishi kama Dorkasi
Matendo 9;36-42
·
Utaongeza
thamani ya maisha yako mbele ya Potifa kama Yusufu
·
Utaongeza
uthamani wako kwa jamii yako kama Daudi
1samweli 17;34
Biashara
yeyote ile utakayoifanya ikagusa maisha na matatizo ya watu ni lazima
itakuletea matokeo makubwa ambayo yatavunja mipaka ya maisha yako.
5.KANUNI YA TANO.
ONGEZA UWEZO WAKO.
Ili uweze kuvunja mipaka
yako[limitations]hakikisha unatumia nguvu kubwa zaidi kuliko zile ulizozitumia
awali
Mfano kama wewe ukitaka kuwa na uwezo
wakutunisha sana misuli yako utalazimika kunyanyua jimu zito kuliko lile ambalo
umelizoea kwa sababu kwa kadri unapozidi kunyanyua nzito zaidi ndivyo
unavyozidi kuongeza ukakamavu wa misuli yako
Sasa ongeza uwezo wako
·
Soma
sana vitabu
·
Fanya
mazoezi sana ya viungo
·
Fanya
mazozi ya kupiga chombo cha muziki ukipendacho
·
Fanya
mazoezi ya kufundisha
·
Jiendeleze
sana kiujuzi
Unapofanya mambo haya yatakusaidia kuweza kuvunja mipaka katika
kila kitu unachokifanya.
Usikose kuendelea kufuatilia masomo haya kutoka
ONLINE GOSPEL SERMONS[OGS]
+255621029725/+255677904755.
OGS WHATSAP,YOU TUBE,INSTAGRAM NA FACEBOOK
No comments