KANUNI ZA KIVITA!-BATTLE PRINCIPLES!
KANUNI ZA KIVITA!
Na Mwal.Chavala PM Ezekia.
Vita inapokuwa inaendelea huwa kuna
kanuni na masharti ambayo muhusika [wahusika wa hiyo vita watatakiwa kuyafuata.
Tofauti na hivyo utajikuta umekosea
masharti na hatimaye ukauawa kabla hata vita yenyewe haijachanganya na kuwa
kali
Unaweza ukafa kizembe sana vitani
tena bila hata kujitetea kwa sababu tu umekosea masharti madogo madogo.
KANUNI YA KWANZA.
USIFANYE KITU CHOCHOTE
BILA KUELEKEZWA
Waliotengeneza muundo wa uwepo wa
makamanda au viongozi wa kijeshi walikuwa na maana kubwa sana ,maana walitambua
kuwa ,asipokuwepo kiongozi hawa wapambanaji wanaweza kujikuta wanapigwa bila
utaratibu wowote.
Sasa usipofuata maelekezo utajikuta
unaenda kinyume na wenzako na ukawa hatarini kuuawa .
Mfano.
Kama kamanda atawambia retreat halafu
wewe ukaendelea mbele kupambana utakuwa peke yako na hapo utapigwa kisawa sawa
Hata ki Biblia bado hali kama hii
inaweza ikakufanya ukakosana na watu kwa sababu umefanya kitu ambacho Mungu
hajakuagiza ufanye
Matendo ya mitume 7;22-27
Hapa utakutana na Musa kabla hajapewa kazi rasmi na Mungu
alijifanya anaanza kuwaokoa ndugu zake wa kiebrania waliokuwa wanapigana,na
kuna sehemu alimuua kabisa Yule mmisri aliyekuwa anamtesa mwebrania,hii ilikuwa
hasira ya Kimungu ndani yake,lakini hakuwa tayari amepewa maelekezo ya kufanya
vile ,kwahiyo matokeo yake wale waebrania wakamsema na kumchukia
Angalia mstari wa 27
Hata kama kitu unachokifanya ni
kizuri lakini nkama usipofuata maelekezo ukajifanyia mwenyewe kwa kiherehere
chako utaishia kuonekana mbaya hata kama lengo lako lilikuwa ni jema
KANUNI YA PILI!
USISEME KITU KAMA
HUJAPEWA RUKSA YA KUSEMA
Kuna watu tunasema ni
vipele[yaani wanapenda kuropoka ropoka sana
Hata kitu kidogo tu
kimetokea katika maisha yao watatamani kumueleza kila mtu
Inawezekana kabisa
lengo lao likawa ni jema kabisa ,lakini je ni lazima useme?
Kuna maeneo katika maisha umejikuta
unaongeza idadi ya maadui zako ,sio kwa sababu hawakupendi hapana ,ila kwa
sababu wewe umetangaza na kusema mambo Fulani hususani yanayo kuhusu hata wewe
mwenyewe
Kuna dogo mmoja anaitwa Yusufu katika
Biblia,alichukiwa sana na ndugu zake [kaka zake ]kwa sababu ya tabia ya
kujitangaza tangaza kila hatua anayoipitia
Angalia
MWANZO 37;5
‘‘Yusufu akaota
ndoto,akawapa ndugu zake habari,nao wakazidi kumchukia’’
Unapokuwa na maono
Fulani usipende kumtangazia kila mtu,wakati mwingine unasababisha vita yako ya
kuyapata maono hayo ikawa kali zaidi kwa sababu ya ule upinzani utakaokutana
nao kutokana na watu wenye wivu dhidi yako.
FAIDA ZA KINYAMAZA! HATA
KAMA UNAVYO VYA KUSEMA
·
Utapunguza idadi ya
maadui wanaokuonea wivu
·
Utamchanganya adui yako
asijue mipango yako ya kivita
·
Utamfanya adui yako
akose mbinu ya kukushambulia[comfussion of your enermy]
KUWA
MKIMYA KAMA SIO LAZIMA USEME
MIMI
NINGECHAGUA KUNYAMAZA ..WEWE JE?
Endelea
kufuatilia Online Gospel Sermons articles
Pia
fuatilia Facebook page yetu[GOSPEL SERMON MINISTRIES]
Instagram/Ezekia
_Chavala
Call
us today
+255621029725
No comments