UVUMILIVU

Shalom

Ujumbe wetu wa leo

*OGS-2020-21*
*UVUMILIVU*

Shalom watu wa Mu
ngu.
Katika sermon yetu ya leo ,nimepata kibali cha kuzungumzia mada hii ya *uvumilivu*

Tuanzie hapa🤔

Nataka nikupatie maana chache za uvumilivu

 *Uvumilivu ni;*

1⃣Ile hali ya kuendelea kufanya jambo uliloamua kulifanya hata kama kuna mazingira yanagoma kiasi gani ..

Kuna namna mazingira yanakatisha tamaa sana ...sasa unapokuwa na uwezo wa kuendelea kusukuma hilo jambo hata katika mazingira magumu kiasi hicho...huo ndio uvumilivu( sustainability)
Uendelevu

2⃣Ile hali ya kutokatisha kitu unachokifanya kwa sababu zozote zile ..ziwe nzuri au mbaya.

Mfano
Umeamua kuanza kujenga utaratibu wa kujisomea kwaajili ya kupanua uelewa wako ...mara ghafla mwanao anafungulia kipindi kizuri sana cha tamthiliya kwenye TV yako...kama endapo utaamua kuondoka na kitabu chako kwenda chumbani au barazani ukaendelea kujisomea ukaacha tamthiliya ikupite basi huo ni uvumilivi tena babu kubwa


3⃣ni ile hali ya kuona mapungufu ya ndugu yako au mumeo au mkeo,lakini bado ukasema labda atabadilika na mwingine akasema ...hata asipobadilika siwezi kumfukuza..nitaishi nae tu hivyohivyo- ni ile hali ya kutoruhusu mapungufu ya mtu au kitu kikuharibie mahusiano baina yako na ndugu zako wa karibu

Huo ni uvumilivu


 *Baada ya kuangalia definition hizo chache sasa naomba tuone  umuhimu wa uvumilivu*

🔰uvumilivu huleta mafanikio

Hata waswahili wanasema ...mvumilivu hula mbivu

Kuna mambo ambayo hautakuja ufanikiwe katika maisha yako kama ukiwa ni mtu wa kukata tamaa haraka..

Moja ya siraha pekee ya kuitumia ili ufanikiwe ni uvumilivu

✍🏼kuna baadhi ya mambo ambayo ukianza kuyatekeleza matunda yake hayaji kwa muda mfupi
Utalazimika kusubiri kwa muda mrefu sana ndipo uone matokeo

Kama usipokata tamaa mapema ...utayaona matunda ya uvumilivu katika kila kitu unachokifanya kilichochema


🔰uvumilivu hupunguza gharama..

Hebu jiulize swali hili...mfano wewe ni mkulima...umepanda mbegu ya aina fulani shambani mwako..ila kwa kukosa uvumilivu unahisi kama inachelewa kuota ..unaamua kubadilisha aina ya mbegu na kupanda mazao mengine

Mwisho wa siku utajikuta  umetumia gharama kubwa ..lakini matokeo ni kidogo

Hata ukiwa wewe ni mwanafunzi..ukawa umesoma Engeneering mwaka wa kwanza..ukakuta ngumu..ukasoma Medicine mwaka mwingine ukakuta ngumu ..ukasoma sheria na kuendelea..baada ya muda utajikuta umetumia gharama kubwa sana kufanya kitu kilekile na bila mafanikio..
Kumbe kama ungekuwa na uvumilivu ..usingepoteza gharama nyingi kiasi kile


🔰uvumilivu hulinda amani na upendo

Kama kuna kitu ambacho kinalinda amani baina ya watu ni uvumilivu

Mfano mzuri ni kwa wanandoa...ikitokea mmoja kati yao hana uvumilivu ni rahisi sana amani ikaondoka na kutoweka kabisa katika familia

Lakini kupitia hii siraha ya *uvumilivu* kuna mambo mengi yanapotezewa tu na unajikuta maisha yanaenda

Kuna watu wamepoteza wapenzi wao...wake na waume zao,,ndugu zao,,na hata kazi zao kwa kukosa uvumilivu


Kila jambo lina wakati wake
*Muhubiri 3:1-5*
Lakini kinachokufanya uendelee kusubiri wakati sahihi wa kila kusudi ni ule uvumilivu wako


Yawezekana saizi ulitakiwa kuwa mbali sana katika hicho unachokifanya ...shida yako ni kwamba ..aiku ulipoanza ukaona kama vile hakuna matokeo uliyoyatarajia  kwa haraka ...ulikata tamaa..na baada ya muda ukaanza tena..hivo unajikuta umedumaa katika hicho..

Unatakiwa kuwa mvumilivu sana ..maana uvumilivu utakupatia chance ya kupata mafanikio na kuwa kielelezo na kwa wengine


Biblia katika Galatia 5:22
Inautaja uvumilivu kama moja kati ya matunda ya Roho mtakatifu

Pasipo uvumilivu kuna mambo mengi sana yanaweza kukwama katika maisha yako

Mungu akubariki
Endelea kuwa mvumilivu

Na Mwal..Ezekia Paul Chavala
Online gospel sermons
0621029725-direct

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.