UTOSHELEVU KATIKA MAPUNGUFU
✍🏼Hakuna kitu kinauma moyo sana ..kama kuambiwa kuwa hautoshi katika eneo uliopo
💥Mtu akikwambia kuwa hautoshi..kwa lugha nyingine amemaanisha hauwezi
🔥Kuambiwa hauwezi ni kitu kinachovunja moyo sana
Japokuwa kuna wakati Kweli unakuwa hautoshi
😟Maana ukweli mwingine unauma lakini ndio ukweli sasa ..hauwezi kuukataa
➖Je Mungu anafikiriaje kwa habari ya utoshelevu(kutosha)??➖➖➖➖➖➖➖
2korintho 3;5
5 Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu.
1⃣Kibinadamu kuna maeneo kwakweli hatuna sifa kabisa..yaani kwa lugha nyingine tunapwaya sana...lakini
MUNGU NDIYE ATUTOSHELEZAYE
Kwa maana anaficha madhaifu yetu na kutufanya tuonekane bora
2⃣sio kika siku ukipigiwa makofi ni kwa sababu umefanya vema
kuna wakati Mungu ameamua kukuhifadhi usitie aibu tu ..ila kiukweli umeharibu

Sasa unatakiwa kuwa mnyenyekevu maana kuna nyakati Mungu atakupatia kibali ..pamoja na mapungufu yote uliyonayo...usiseme ni kwasababu ya akili zako au unaarufu wako
❌Dont even think about that! Usiwaze kabisa kujiinua wala kujisifu
Ndugu Neema ya Mungu ndiyo imekufanya uonekane kama Unatosha hapo..ila Behind the scene..uko shallow sana yani😕😕
👀👀ulishawahi kuangalia kwa jicho la nne ..namna ambavyo Musa alipewa kazi ya kwenda kuwatoa wana wa Israel Misri,halafu baada ya muda akaanza kutaka kuonesha kama na yeye ni miongoni mwa ile miujiza aliyokuwa anaifanya Mungu kule jangwani?
➖wanadamu tulivyo wasahaulifu➖
😕Jamaa alisahau kabisa kuwa hata kuongea hakuwa anajua..ndio sababu Mungu alimruhusu Haruni walau awe msemaji kule kwa Farao
✍🏼Neema ya Mungu ndiyo inakufunika hata hapo ulipo leo..
💥unatakiwa kuwa mnyenyekevu sana maana UTOSHELEVU WETU WATOKA KWA MUNGU
Nikutakie siku njema ..
Yenye utoshelevu wa Mungu
Mwal.Chavala PM Ezekia
Online gospel sermons
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments