KANUNI ZA MAFANIKIO YA KWELI
Shallom namshukuru Mungu tena kwa siku hii ya tatu ya semina yetu maana tunajua
wote ni kwa neema tu, karibu basi tuendelee na kanuni nyingine.
🙏🏻🙏🏻MSAMAHA (forgiveness)
Wakati najiandaa na somo hili, mtumishi wa Mungu E chavalla alikua akitufundisha somo lililoitwa JERAHA LA MOYO ubarikiwe sana chavalla kwa kutumiwa na Mungu kuponya majeraha mengi. Sasa lile somo limeendana kidogo na hili la leo.
👉Tunapoendelea na maisha wakati mwingine tunapitiwa tunafanya makosa, maana sisi ni binadamu na tupo fallible kwa asili, sio malaika. Makosa hayo yanaweza yakatokea kwenye mahusiano, biashara au kwenye kufanya maamuzi ya kawaida.
👉👉Kutosamehe kutakufanya uteseke sana kwenye maisha.
Niliwahi kukutana na rafiki yangu Fulani aliyekua akijutia sana maamuzi yake ya kutaka kuoa. Maana alimchumbia msichana Fulani na alijitoa sana kwenye mahusiano yale
Lakini baadae msichana akakataa kuolewa na yeye na kwenda kuolewa na mtu mwingine 😖😖
Jamaa alijisikia vibaya sana maana mahusiano yamekwisha na bado anafikiria yule msichana alikua ndio sababu ya yote hayo.
👉👉Kwa kweli ni kawaida kabisa kujisikia vibaya wakati unakosewa Lakini ukweli ni huu 👉👉kama hutasamehe na kusahau huwezi kurudi na kuishi maisha yako tena ( you will never have your life back) kila siku utaishi kwenye kile jeraha inamaana utaishi maisha ya nyuma huwezi kwenda mbele na kwa kufanya hivyo huwezi kufanikiwa huwezi kuwa yule mtu ambae Mungu anataka uwe. Mungu sio kwamba hana akili aseme anatusamehe dhambi zetu kwa ajiri yake, kwa sababu anajua asipotusamehe sisi mbingu hazitakua na furaha zitahuzunika tu watu wakifa kwenye dhambi. Hebu na wewe. Jifunze kusamehe kwa ajiri yako mwenyewe.
👉👉 Unaweza kuona kutosamehe kutakuathiri wewe zaidi kuliko yule aliyekukosea, wewe ndiye unayetembea na uchungu mwenzako anaendelea na maisha yake. Ule uchungu unaotembea nao sasa ni lazima ukuathiri kiroho na kusaikolojia, utaathiri pia ile quality ya mawazo yako na level ya uzalishaji wako pale kazini kwako. Unapoachilia mambo unapata utulivu na utafanya shughuli zako kwa usahii zaidi.
👉👉 Inatokea boss umekwazwa nyumbani ukienda huko kazini ni kuvumbi na jasho 😀😀uso umekunjamana kila mtu utamwona mbaya kwako noo hebu samehe kwanza na uachilie kabisa ili ufanye shughuli zako saaaafi kabisa.
Nanyi mkiwa katika kusali salini hivi ".............utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu". Mathayo 6:12, asante tukutane tena wakati mwingine. Barikiwa sana
E J MWORIA
ONLINE GOSPEL SERMONS
No comments