KANUNI ZA UONGOZI


    
                  KANUNI ZA UONGOZI
           Na mwalimu Chavala PM ezekia.





Katika somo hili tutajifunza mambo yafuatayo
1.Utangulizi
2.Sifa za kiongozi


                             Karibu sana Katika somo hili.!

SEHEMU YA KWANZA

UTANGULIZI;

Kiongozi ni nani?
Watu wengi wamekuwa hawataki kabisa kujifunza habari za uongozi,na imekuwa hata ukitaka kufundisha habari za uongozi ,kila mtu asiye na madaraka Fulani katika taasisi Fulani anakimbia hilo darasa akidhani ya kuwa yeye somo hili halimhusu.
Kupitia somo hili nataka nikufungue katika eneo la akili yako uweze kujua kuwa kiongozi ni nani
Katika Misingi ya Kibiblia –Mwanadamu yeyote aliumbwa awe kiongozi
Kwa sababu,kama usipokuwa kiongozi kwa kuanza hata kujiongoza mwenyewe bila shaka hautaweza kutawala viumbe vyote ambavyo Bwana Mungu alivifanya akakupatia mamlaka ya kuvitawala na kuvitiisha
Sasa kabla hatujaenda mbali sana,hebu tuangalie maana za kiongozi


Kiongozi ni nani?
Kiongozi ni mtu mwenye ushawishi kwa watu wengine ili wamfuate yeye na kile anachotaka wakifanye kwa hiyari yao
[Nielewe hapa kwa umakini]
Unamshawishi mtu halafu humlazimishi afanye unavyotaka ila yeye mwenyewe anaona hana sababu ya kutokukusikiliza na kutokufanya kile unachotaka kifanyike
Sasa ili ufikie viwango vya kumfanya mtu au kitu kikutii na kukusikiliza bila kulazimisha ,kuna masharti ya muhimu na kanuni za muhimu ambazo ndizo tutaenda kujifunza katika somo hili.

Mwanzo 1;26
‘‘Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu,wakatawale samaki wa baharini na ndege wa anagani,na wanyama ,na nchi yote pia na kila chenye kutambaa,kitambaacho juu ya nchi.’’
Kupitia somo hili naomba sasa nikupe maana za kiongozi kibiblia.
1.Kiongozi ni mtu aliyepewa mamlaka na Mungu ya kutawala viumbe vyote
[samaki,wanyama,ndege,na kila kitambaacho]
Sasa kama ukiona kuna namna viumbe hawa hawakutii wewe jua umepoteza moja ya sifa [drive]za kiuongozi!


Kwa sababu hawa wote ni lazima wawe chini yako ,na hawawi chini yako kwa kuwalazimisha ,hapana ila  wewe mwenyewe kuna sifa unatakiwa kuwa nazo ambazo zitawafanya wote wawe chini yako ,nitazieleza hapo baadaye.
Mfano
Siku moja wakati naanza kazi ,nilikuwa nimepanga nyumba eneo Fulani,sasa lile eneo lilikuwa na kichuguu cha siafu b,kwahiyo usiku siafu waliingia nyumbani kwangu,wakaleta kero sana kwangu na panoja na kwenye vyumba vya wapangaji
Mimi nikasema moyoni mwangu,inawezekanaje viumbe ambao nimepewa mamlaka dhidi yao [mimi nikiwa kiongozi wao]wanakuja na kuniletea usumbufu bosi wao?
Niliamua kuanza tu kuwambia kwa upole kuwa ENYI SIAFU,MIMI NI BOSI WENU,HAMTAKIWI KUWA NDANI KWANGU,NENDENI NJE KATIKA JINA LA YESU SIWAHITAJI HAPA NDANI NINAWAAMURU!

Kuna mtu anadhani nafanya utani lakini ndio uhalisia wa kilichotokea,nadhani Bwana alikuwa ananifundisha somo la uongozi hapa
Baada ya muda kweli wale siafu wakaanza kuondoka ,ni kama mchezo wa kuigiza nikaona wanahama kwenye chumba change wakaendelea kuwasumbua wapangaji wenzangu
Text Box:     NI MTU MWENYE MAMLAKA DHIDI YA VIUMBE WOTE WA KIBAYOLOJIA
m
Hii ndio maana ya kwanza ya kiongozi








                                                         
2.Kiongozi ni Balozi wa serikali anayoiwakilisha
Naomba kupitia mfano huu,unielewe vizuri zaidi kwa jina la Bwana.
Unapokuwa kiongozi maana yake unawakilisha serikali husika unayoiongoza.sasa Serikali ni taasisi Fulani ambayo inatekeleza malengo mbalimbali iliyojiwekea ,
Wewe Binafsi una serikali,ndiyo maana una uwezo wa kufanya maamuzi kitu gani ufanye na kitu gani usifanye
Mtu gani umsalimie na huyu usimsalimie
Mtu gani umchukie na yupi umpende
Yupi awe rafiki yako na yupi awe adui yako
Haya maamuzi yote yanafanywa na wewe,kwa bahati nzuri kumbe wewe ni kiongozi wa kwako mwenyewe,lakini pia unaweza kuwa kiongozi wa serikali za kidunia na wakati mwingine ukawa kiongozi wa taasisi mbalimbali za kidini ,na kikanisa,
Sasa kiongozi ni balozi wa serikali anayoiwakilisha





SIFA ZA BALOZI YEYOTE
·         Lazima ajue Nchi anayoiwakilisha[serikali anayoiwakilisha]
Huwezi kuwa Balozi wa Mungu kama humjui Mungu

·         Ni mtu mwenye mawasiliano ya moja kwa moja na serikali anayo iwakilisha
Huwezi kuwa unamwakilisha Tanzania Marekani ,halafu usiwe na mawasiliano na Raisi wa TANZANZIA,
Unapokuwa Balozi unakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na serikali yako

[Ki biblia sisi tuliomwamini Yesu tunakuwa viongozi[mabalozi wa ufalme wa Mungu na hivyo tunayo nafasi ya kuwasiliana na Mungu Moja kwa moja]

2korintho 5;20
‘‘Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo kana kwamba Mungu anasihi kwa Vinywa vyetu’’
·         Ni mtu mwenye siri za serikali anayoiwakilisha
Zaburi 25;14
Siri za Bwana ziko kwa wamchao nae atawajulisha Agano lake
Kwa sifa hizi chache za Balozi tunapata maana ya pili ya Balozi kuwa





SEHEMU YA PILI
SIFA ZA KIONGOZI
Zifuatazo ni sifa za kiongozi yeyote Yule




1.KIONGOZI LAZIMA AWE JASIRI
Sasa ukikuta mtu ni kiongozi wenu lakini hana ujasiri ,basi tambua kabisa huyo kuna vitu vya kiuongozi amevipoteza ,hatakiwi kuendelea kuongoza
Kiongozi yeyote ni lazima awe jasiri wa;
·         Kufanya maamuzi magumu
·         Kukabiliana na maadui kwaajili yake na kwaajili ya anao waongoza
1samweli 17;45-46
Katika fungu hili utaona Daudi anavyompatia sababu za yeye kumpiga Yule mfilisti
‘kwaajili ya waisraeli uliowatukana’ akamtandika kisawasawa!





2.KIONGOZI LAZIMA AWE  NA MSIMAMO
Hii inamaanisha kuwa ,uwe na uwezo wa kusimamia kile ulichokiamua
Tumekuwa na watu wengi ambao hawawezi hata kujisimamia wenyewe,inakuwa ni kero sana hata katika familia
Mfano,mume au mke ambaye hana msimamo hata siku moja hamuwezi kufanya mambo ya maendeleo mkavunja mipaka na kwenda ngazi nyingine
Lakini pia kukosa msimamo binafsi ndiko kunakopelekea watu waweze kutangatanga katika maono waliyo nayo
Leo anawaza kufanya hiki na kesho anabadilisha anafanya kitu kingine
Leo anaamua kuwa taasisi yenu mtafanya hiki lakini kesho anabadilisha mawazo anawapeleka kwingine kabisa!
Haitakiwi kiongozi yeyote akose msimamo.
Daniel 1;8
‘‘Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme wala divai aliyokunywa……………………………’’
Katika mazingira yeyote yale hata iwaje msimao wa kiongozi  unatakiwa uwe katika kusimamia haki na kile anachokijua, hatakiwi kuyumbayumba .




3.AWE NI MTU WA KUJITOA NA KUFANYA KWA MOYO KILE KITU ANACHOKISIMAMIA
[PASSIOANTE]
Kiongozi mzuri ni Yule ambaye anaupenda uongozi wake kwahiyo hata kama mazingira yatakuwa ni magumu sana ,hawezi kuacha kufanya kitu ambacho kiko moyoni
Kwa lugha nyingine
Lazima aweze kujitoa kwaajili ya wengine
Katika ile 1 samweli 17;45
Kilichomfanya Daudi ajitoe kwenda kupigana na Goliath sio kwa sababu alitakiwa kwenda kule ,kwanza hata hakuwa na lile jukumu,ila kwa sababu alikuwa na ile passion ya ndani ya kufanya kile kitu ndiyo maana aliamua kujitoa na kwenda kupigana na Goliath.




4.AWE NA UTU[HUMILITY]

Sifa nyingine nzuri zaidi ya kiongozi ni ile hali ya utu [kujali utu wa wengine]
Unapokuwa na huruma unaonesha sura kamili ya Bwana wetu Yesu na ndio maana moja ya dalili kwamba Mungu anakuita ufanye kazi yake utajikuta umeanza kuwa na uchungu sana na watu wanaopatwa na matatizo      na wanaokufa katika dhambi,kuna muda hata machozi yatakutoka kwaajili yao
Hii ni ishara tosha kuwa Bwana anataka uwe kiongozi bora wa kuwahudumia watu wengine
Lakini pia katika familia kusipokuwa na ile huruma ya kiutu [humility familia itapata tabu na shida sana ]
Kiongozi bora lazima awe na utu wa kuwajali watu wa aina zote na makundi yote.
Mfano
Unadhani ni kwanini Yusufu alilia pale alipojifanya hawajui wale kaka zake walipokuja kununua nafaka Misri wakati huo yeye akiwa ni waziri mkuu?
Biblia inasema Yule dogo alikuwa akiongea nao anajifanya yuko ngangali sana lakini anatoka anaenda chumbani analia sana kwa uchungu
Huo ndio ule utu wenyewe
Soma Mwanzo 43;30 na MWANZO 45;1-3
Ukiona kuna muda hadi unapatwa na machozi kulia kwaajili ya watu wengine ,au ndugu yako jua umeanza kuwa na sifa za kuwa kiongozi.




5.HEKIMA YA KUFANYA MAAMUZI
Uongozi wowote unahusisha sana ufanyaji wa maamuzi
Hauwezi kuwa kiongozi mzuri kama unafanya vibaya katika kutatua changamoto za watu
Watu wanakuja kujiuliza kwako mambo mengi yanayohusu maisha yao lakini wewe unatoa maamuzi ya hovyo huna sifa za kuwa kiongozi.
Kiongozi anakuwa amejaa  hekima ya MUNGU ya kumwezesha kufanya maamuzi sahihi kama Suleimani



Mithali 8;11
‘‘Maana Hekima ni bora kuliko marijani,wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo’’
Sasa hekima kwa lugha nyingine ni uelewa wa Neno la Mungu utakaokusaidia kujua uamue nini hata katika maombi yako useme nini,uwashauri nini watu na vingine vingi!
Unapokuwa na hekima ya Kimungu kuna vitu viitaanza kukutii kwa sababu mamlaka yote unaipata unapokuwa na ile hekima ya kimungu Ndani yako!
 Ayubu 28;12.



Usikwepe kuwa
 kiongozi,usipotaka kujifunza uongozi utashindwa hata kujiongoza mwenyewe
Mungu akubariki sana
Endelea kufwatilia masomo yetu kutoka Online Gospel Sermons yanayokujia kila siku
You tube,Face book page,Blog yetu ya online gospel sermon[ogs] NaWhatsap group la OGS
Mr Chavala PM ezekia
Call+255621029725/+255677904755
MUNGU AKUBARIKI!

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.