Power of your possession
SEMINA YA NENO LA MUNGU
THEME: *THE POWER OF YOUR POSSESION-NGUVU YA UNACHOKIMILIKI*
TAREHE; *20/1/2020*
*Mwal.Chavala Ezekia Paul*
✍🏼UTANGULIZI
Kila kitu unachokimiliki huwa kina uwezo wa kukuletea matokeo ya aina mbili tu
1⃣kukuinua(promote)
2⃣kukuharibu( Destruct)
Haya ni matokeo ambayo huwezi kuyakwepa maana kwa vyovyote vile ni lazima mojawapo likupate
*Mfano*
Ukimiliki gari; linaweza kukufanya aidha ukawa masikini kwa sababu ya gharama za uendeshaji ,au ukawa tajiri kwa sababu ya matumizi sahihi yenye tija katika maisha kwa kupitia gari lako
*Mfano 2*
Ukiwa na mke au mumeo
Anao uwezo wa kukufanya aidha uone Dunia ni mahali sahihi pa kuishi kwa amani kama mbingu ndogo😅😅
Au
Anaouwezo wa kukufanya uone Dunia ni jehanamu ndogo unapoisubiri iliyokubwa😌😌😌
Sasa kwa mifano hii unaweza kuona kwa kila unachokimiliki ,huwa kuna nguvu ya ndani ya aidha kukuletea matokeo chanya au matokeo hasi
*Mfano 3*
Unaweza ukapata watoto katika ndoa yako,lakini watoto wako wakafanyika mwiba katika maisha yako hadi ukajuta ni kwanini Mungu alikupatia watoto
Lakini pia ..unaweza ukapata watoto halafu watoto hao hao wakakufanya uone furaha ya kuwa nao
✍🏼kati ya watu ambao ninadhani walipata shida sana na pengine walijilaumu sana kwa matokeo yaliyosababishwa na wanavyovimiliki ninadhani mmojawapo ni *ADAMU*
*MWANZO 3:1-7*
BIBLIA inaeleza kwa habari ya majanga makubwa ambayo mpenzi wake Adamu aliweza kumsababishia mumewe pamoja na yeye
Ni baada ya kudanganywa na nyoka na hatimaye akavunja sheria za pale Edeni ..mwishowe wanafukuzwa kukaa Edeni na kupewa adhabu ya kula kwa jasho tofauti na zamani
Mfano mwingine ,ni mpenzi wake Samsoni ..yaani Delila..nayeye pia aliweza kuonesha namna ambavyo kile ulichonacho kina uwezo wa kukusababishia mema au mabaya katika maisha yako🖕🏽
Sasa hiyo ni baadhi tu ya mifano ..lakini unaweza kuolewa na mwanaume ambaye akabadilisha kabisa Historia ya maisha yako kwa tabia zake..mbaya...hali kadhalika unaweza kuoa mwanamke ambaye kwa tabia zake akabadilisha kabisa historia ya maisha yako
Haya yote yanaweza kukuletea matokeo chanya au hasi
✍🏼sasa kila unachokimiliki kinao uwezo wa kukuletea matokeo chanya au matokeo hasi!!
*The power of your possesion*
Kitakachopelekea matokeo haya yawe mazuri au mabaya ni ule uendeshaji wa kila siku wa hicho kitu chako..
Namna *unavo kihudumia*
Sasa kabla hatujaenda kwenye sababu zinazoweza kupelekea unachomiliki kikuletee matokeo mazuri au mabaya,naomba nikupitishe kwanza kwenye *Sheria za umiliki*
2. *SHERIA ZA UMILIKI HALALI*
Rafiki yangu ,ukitaka kuwa mmiliki halali wa hicho ulichonacho,ni lazima sheria hizi zitumike kwako..
🔰 *Ni lazima ugharimie unachokimiliki..*
Hujawahi kuona mtu amekaa amenyang'anywa viwanja au mashamba hata kama amevitumia kwa muda mrefu..ila kwa sababu hajavigharamia kwa kuvilipia na kupewa hati yake kisheria..anajikuta ananyang'anywa na anakosa uwezo wa kudai maana hana vithibitisho kuwa alivyonavyo ni vya kwake!
Ili uweze kuwa mmiliki halali wa ulichonacho..hakikisha umegharimia kihalali na umelipa gharama zote za msingi..na una hati
*Yeremia 32:9*
Huyu jamaa alinunua shamba ..na akalipa gharama ya lile shamba na akapewa na hati yake
*Mwanzo 23;16-18*
Ibrahimu nae alinunua shamba na akalipa gharama ..fedha ...halafu akapewa na hati yake tena mbele ya mashahidi
Nimeona tuanzie hapa ili tuwe na uhalali wa tunavyo vimiliki kabla ya kuingia kwenye namna ya kuvifanya vituletee matokeo makubwa na chanya katika maisha yetu
Ndugu yangu mpendwa
Hakikisha kuwa kila kitu unachokimiliki una hati halali ya umiliki wako na usifanye vitu kwa magendo..maana ipo siku vitakuja kukuletea matokeo mabaya sana katika maisha yako na utashangaa.
🔰 *uwepo wa mashahidi halali*
Kila unachokimiliki hakikisha kuna mashahidi ..watakaojua kuwa kwa hakika kile kitu ni mali ya kwako
Baada ya semina hii kuisha nataka uanze kutafuta na kurasimisha kila kitu ulichonacho kwa kutafuta vielelezo halali
Maana kuna wazazi wengi wanakufa halafu wanaacha familia zao zinakaa katika misukosuko kwa sababu ya migogoro ya umiliki wa vile wanavyo viacha
Unapokuwa na mashahidi halali wa vile unavyomiliki ni rahisi sana kuweza kumaliza mgogoro maana kazi ya mashahidi ni kutoa uelekeo wa nani mwenye haki katika kesi
Make sure unatafuta mashahidi tena kwa maandishi katika kila kitu ulicho nacho...hii nayo ni biblia
Yeremia 32;9-10
Mwanzo 23;17-19
Kila unachokimiliki..weka na ushahidi
Yaweza kuwa ni hati miliki ,watu wa karibi tena mkaandikishana nk.
Nasema haya kwa sababu tunakokwenda kile ulichonacho kitaenda kukuletea matokeo makubwa mazuri baada ya kumaliza hii semina..sasa ninakutengenezea msingi ili kwamba utakapofanikiwa asiwepo wa kukusumbua katika umiliki wako..
🔰 *Kiguse maisha yako*
Kitu chochote ambacho hakitagusa maisha yako..hauna sababu ya kukimiliki
Mfano
Mwanamke mwenye mimba huwa anambeba mtoto wake kwa uchungu ..anamzaa kwa uchungu..hata kama mimba yake itamsumbua..atatapika tapika sana ..hadi hatimaye atamzaa mwanae mpendwa
Namna alivoguswa na yale maumivu wakati wa kujiandaa kuzaa...huwa kunampatia mwanamke yule ule umiliki halali na wa ndani sana..hatimaye anajikuta kwakweli anamlinda na kumtetea sana mtoto wake
*Mathayo 1;25*
Mariamu anakuwa mmiliki halali wa mtoto Yesu kwa sababu ya ile gharama ya kumbeba Yesu miezi tisa tumboni ...hadi akazaliwa
Unapata ile hali ya kujali ulichonacho kwa sababu ya ule mguso wa kimaumivu uliyoupata wakati unajiandaa kukimiliki hicho kitu
Kwa lugha nyingine
Unapopambana na kuumia sana kutafuta ,ndipo utakapokipata utakuwa na ile hali yabkukijali na kukitunza kile ulichokipata..
✍🏼sasa baada ya kupitia baadhi ya kanuni muhimu za umiliki halali sasa naomba
nikupeleke moja kwa moja kwenye sehemu ya tatu ambayo ni
*3.MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA ULICHONACHO KIKAKULETEA MATOKEO AIDHA CHANYA AU HASI*
Baada ya kuwa nimezungumzika habari za sheria za umiliki halali .sasa naomba nikupitishe katika mambo ambayo yanaweza kukuletea matokeo aidha chanya au hasi katika maisha yako
1⃣ULINZI(PROTECTION)
Chochote unachomiliki huwa kinaleta matokeo aidha mabaya sana au mazuri sana kutokana na hali ya ulinzi ulio elekeza kwa kitu hicho
*Mwanzo 3:1-7*
Adamu alishindwa kumlinda mke wake..matokeo yake mkewake kakutwa na nyoka(shetani) kapata nafasi ya kumdanganya
Protection ni ile hali ya uangalizi wa karibu katika kila kitu cha kwako
Kwakweli sitaki kumsema vibaya Adamu..ila nataka tujifunze tu kupitia makosa aliyoyafanya yakasababisha mke wa kwake mwenyewe amtenge na Mungu ..na kuleta majanha katika maisha yake
Pata picha kama Adamu asingemwacha yule mkewe azulule zulule peke yake! Unadhani angepata nafasi ya kudanganywa na nyoka kama muda wote yuko na Adamu?
😃😃😃😃😃😃😃😃
Kuna wakati watu wanajikuta wake zao au wapenzi wao wamewasaliti..na kuwaletea matatizo katika familia zao ..ukweli ni kwa sababu ...moja ya sababu ni kutokuwa beneti nao
Yani wewe uko na mke ..halafu unamuacha miezi na miezi hauko karibu nae..siku akikuletea mtoto mzungu usishangae ..ni matokeo ya kuto mlinda..kutokuwa beneti na mumeo..au mkeo au mpenzi wako...
*Mathayo 2;13-14*
Kuna jamaa wanajua kulinda kwa gharama zote bana
Hapa utakutana na Yusufu na mariamu ..ambao waliamua kumlinda Yesu wao(mtoto wao)
Kumbuka hapa tunamchukua Yesu kama mtoto aliyezaliwa katika familia ya Yusufu..na wajibu wa wazazi kwa watoto wao ..ni kuwalinda..
Kama hautachukua muda kuwalinda watoto wako..usishangae kuja kuona watoto wako wameuawa..na maadui au wamekuwa na tabia mbaya zitakazo kuumiza mwenyewe
*Kila unachomiliki ili kikuletee matokeo mazuri hakikisha unakilinda na kukitunza*
*2⃣KUTOA MAHITAJI( HUDUMA) PROVISSION*
Narudi tena palepale..usipoamua kuhudumia familia yako ...(unachomiliki)
Usishangae siku moja kukuta wenzako wamekusaidia baadhi ya vitu..
Yawezekana kulikuwa na matunda mengine matamu na yenye kupendeza kwa macho zaidi ya matunda ya ule mti wa mema na mabaya katika ile bustani ya Edeni..
Lakini yamkini Adamu hakuwa anapita pita bustanini kuona tunda gani zuri ambalo angelipeleka kwa mkewe ili alifurahie kuwa limetoka kwa mume anaejali
Naomba tujifunze kitu hapa
Mkeo au mumeo anapokosa vitu vizuri ambavyo wewe kwa nafasi yako ulitakiwa kumfanyia...usishangae kuona kuna siku kavipata kutoka nje..ila elewa tu kuwa hivyo vya nje atakavyokuletea vitakuwa na gharama yake ..tena gharama yake itakugharimu kuliko unavyo dhania..
*Mwanzo 3:1-7*
Toa gharama ...hudumia ulichonacho...toa huduma .za uendeshaji wa ulichonacho
Mfano;
Hata gari lako unapokosa kulipatia huduma kama services na matengenezo madogo madogo kwa wakati ..kuna siku litakuja kukugomea eneo ambalo kamwe hautaamini na litakuumiza sana...
Toa huduma kwa unachokimiliki ili kikuletee matokeo mazuri
*Waswahili wanasema*
*Tunza kikutunze*
Usiache kuendelea kufwatilia semina hii iliyoanza leo na itamalizika siku ya jumapili
Kama hujajiunga bado na familia ya OGS
Tafadhari ..usikose mafunzo haya
Bonyeza link hii
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments