THE POWER OF ATTITUDE
NGUVU YA MAWAZO
Mawazo (Fikra) katika nafsi ya mtu ndio uwanja wa mapambano ambapo matokeo ya kinachofikirika huja kuonekana nje katika maisha ya mtu
*💥Kwa bahati mbaya sana.kila jambo unalowaza ,ndilo huja kutokea katika maisha yako kwa nje*
Ukitaka kuthibitisha hilo,jaribu kufikiri wakati ambapo unaruhusu mawazo ya chuki dhidi ya mtu fulani,ndivyo ambavyo mwili wako unaamka na kuanza kumchukia kisawasawa
Mfano
*Ukimuwazia mtu kwa mawazo ya kizinzi au uasherati,ndipo tamaa za mwili huamka na kuanza kutamani kuambatana naye*
Sasa kama haya yanatokea,basi ni dhahiri pia hata ukiwaza mawazo ya mafanikio,mwili pia huanza kurespond kuelekea mafanikio...na pia ukiwaza mawazo ya maendeleo ,mwili huanza kurespond kufanya maendeleo
Ukisoma
*Mithali 10;24*
*Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia; Na wenye haki watapewa matakwa yao.*
Katika andiko hili kuna mambo yafuatayo yamejificha
1⃣hofu huanzia kwenye akili(nafsi)mindset na baadaye matokeo hutokea nje
2️⃣Kama unaweza kujenga hofu ndani halafu ikakuletea matokeo au real image nje...basi pia unaweza kujenga wazo jema ndani halafu likaleta taswira halisi njema nje
3️⃣Tunayoyawaza ndio ambayo hututokea katika maisha yetu,ni heri kuwa na mawazo mema ili tupate mema
Nakutakia siku njema
Ezekia Chavala
Online Gospel Sermons
https://chat.whatsapp.com/DbAV3xNVaEkH0VWoLPlVGW
No comments