JIFUNZE KUPOKEA TAARIFA
NAMNA YA KUPOKEA TAARIFA MBAYA
👉🏾Kutokana na kuwa mwanadamu ameumbiwa nyakati tofauti tofauti
➖Shida
➖huzuni
➖Furaha
➖raha nk.
Kuna muda mimi na wewe tunatakiwa kujiandaa namna ya kupokea taarifa mbaya
*👉🏾Kuna watu wengi huwa wanapata mshtuko hadi wanakufa kwa presha,wengine wanaamua hata kumkufuru Mungu,na wengine kama walikuwa wajawazito mimba zinaharibika ,na wengine wanapatwa na stroke ....kwa sababu ya taarifa mbaya zinazowafikia*
➖natamani kuwa na kifua kama cha Ayubu ambaye wajumbe walimletea taarifa mbaya tenya nyingi kwa wakati mmoja...lakini maamuzi aliyoyachukua ayubu ni kuanguka kifulifuli na kumshukuru Mungu
*Soma Ayubu 1*
*14 mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng’ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao;*
*15 mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.*
*#Habari mbaya ya kwanza*
*16 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.*
👉🏾habari mbaya ya pili
*17 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.*
Alipata habari nyingi zingine zipitie mwenyewe kwa muda wako
*ANGALIA REACTION YA AYUBU BAADA YA KUPATA HABARI MBAYA ZA WAJUMBE*
*20 Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia;*
nakumbuka alishukuru Mungu kwa kusema Bwana alitoa..na Bwana ametwaa Jina la Bwana Libarikiwe
*Wewe na mimi tukoje?*
1⃣tumelaani maisha yetu mara ngapi pale tulipopatwa na mabaya
2️⃣tumemlalamikia Mungu mara ngapi pale tulipopata changamoto tena zenye uwezekano wa kumalizika
3️⃣tulimuona Mungu hafai mara ngapi pale tulipokwama?
4️⃣tulizira mara ngapi pale tulipokosewa?
5️⃣tulikaa chini mara ngapi pale Mungu aliposhindwa kujibu maombi yetu mida tuliotaka sisi
*#Mungu atusaidie sana*
Tukomae kiroho
Nakutakia siku njema
Ezekia Chavala
Online Gospel Sermon
https://chat.whatsapp.com/DbAV3xNVaEkH0VWoLPlVGW
No comments