MSINGI VS MATOKEO

 MSINGI WAKO HUBEBA MATOKEO YAKO



Katika maisha huwezi kupata matokeo mazuri kama msingi wako ni mbaya au mbovu


Na kinyume chake hakuna mtu aliyepata matokeo mabaya kama msingi wake ni mzuri



➖Kila jambo jema linalotokea katika maisha ya mtu ,huwa linaandaliwa 

Na pia

➖Kila jambo baya linalotokea katika maisha ya mtu huwa linaandaliwa...aidha katika ulimwengu wa Roho au katika ulimwengu wa Mwili


Mfano

➖➖➖

👉🏾Ndoa inayovunjika leo ,ni matokeo ya msingi mbovu eneo fulani

👉🏾Ugonjwa unaoumwa leo ni matokeo ya kutozingatia kanuni za afya eneo fulani

👉🏾Umasikini ulionao leo ni matokeo ya kutozingatia msingi wa kanuni za kiuchumi eneo fulani

👉🏾Hali kadhalika mema yote ni matokeo ya msingi mzuri ndipo yanakujia


*Mungu ameweka uataratibu ukitaka kupata mema ufanyaje na ukitaka kupatwa na mabaya ufanyaje*


*Mwanzo 4-:1-4*

Biblia inazungumzia maisha ya ndugu wawili 

Kaini na Abeli


Matokeo waliyoyapata watu hawa kila mmoja yalitegemea sana aina ya msingi aliouchagua kila mmoja


*Abili*

➖Alijiwekea msingi mzuri kwa kutoa sadaka nzuri iliyonona

➖sadaka yake alitoa kwa kumheshimu Mungu maana alitoa wazaliwa wa kwanza



*#Matokeo:Mungu aliipokea sadaka ya Abeli*



*Kaini*

➖alitoa sadaka iliyochoka

➖Alitoa kama vile analazimishwa na wala sio kwa moyo



*Matokeo;*

Sadaka yake haikupokelewa na hivyo akapata wivu akamuua ndugu yake


💥Tengeneza Msingi mzuri ili upate Matokeo mazuri katika maisha yako


Ezekia Chavala

Online Gospel Sermons

11-9-2020

https://chat.whatsapp.com/K3lnh9YaO7Y2Z3SA2MBudI

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.