IF NOT FOR GOD-YOU ARE DEAD

 KAMA SIO MUNGU -WEWE UNGEKUWA WAPI?



➖Kwa namna tunavoishi kama mtu akifungua moyo wako aangalie ulivochoka anaweza asitamani kuendelea kukutazama tena


➖Kwa wastani kwa siku watu wanaokufa duniani kwa sababu ya Covid 19 ni 150000*(wakati wa kipindi cha Corona)


*Sasa kwa idadi hiyo ya watu utaona jinsi familia nyingi zilivojaa vilio,simanzi na huzuni..*.


➖Bado hujaangalia idadi ya ndoa zinazovunjika kila siku na mahusiano au chumba zinazokufa kila siku(ni shida tupu)


*➖Bado hapo hujaangalia watu wanaopata misukosuko kazini na kufukuzwa kazi na kupata kesi nzito zisizo na uwezekano wa kutoka*


Dunia imejaa mikiki mikiki na misukosuko mingi sana...ukiona wewe leo unacheka na kufurahi jua kabisa kuna mtu kama sio jirani yako analia maana kuna mambo kwakwe yamekwama



*💥KAMA ASINGEKUWEPO MUNGU WA KUBALANCE HALI HIZI MBAYA NDANI YETU SISI TUNGEFANYA NINI?*


BILA SHAKA

1⃣Idadi ya wanaokufa kwa presha ingeongezeka zaidi

2️⃣Idadi ya wajane na yatima ingeongezeka zaidi

3️⃣Idadi ya masikini na wasio na kipato kabisa ingeongezeka zaidi

4️⃣Idadi ya watu wanaokufa kila siku ingeongezeka zaidi


5️⃣Idadi ya magereza na mahabusu ibgeongezeka zaidi


*Kwa ujumla matatizo mengi yangetupata na tusingekuwa na sehemu ya kukimbilia*


*#KAMA MUNGU ASINGEKUWA PAMOJA NASI MIMI NA WEWE NA TUSEME SASA*

Tungelikuwa wapi??


*Soma*

Ayubu 4:3 

*Tazama, wewe umewafunza watu wengi, Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge.*


*4 Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge.*



Ifike wakati tutambue kazi kubwa anayoifanya Mungu katika maisha yetu 

➖Kututia nguvu

➖Kuimarisha magoti yaliyolegea

➖Kutufanya upya

➖Kutuhusha tukichoka

➖kuponya afya zetu nk


Nikutakie siku njema 


Mwal.Ezekia Chavala

Online Gospel Sermons

10-09-2020

https://chat.whatsapp.com/K3lnh9YaO7Y2Z3SA2MBudI

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.