FREEDOM !#UHURU UHURU UHURU!

TANGAZO LA UHURU
🇹🇿Na mwal.Chavala PM Ezekia 
💥Hakuna kitu kizuri kinachofurahisha Moyo wa Mwanadamu kama Uhuru.

Uhuru unapokuwepo kuna mambo huwa yanatokea
1️⃣Utaona mtu ana nawiri na kunenepa hata kama hali chakula sana au hali chakula kizuri

2️⃣Utaona uwezo wa mawazo mazuri ya mtu pale unapompatia uhuru wa kujieleza..ndipo utagundua huyu mtu ana vitu vizuri

3️⃣Utaona Bidii ya mtu katika kufanya kazi kwa ubora pale unapomuweka huru..bila kumkandamiza wala kumuendesha 

4️⃣Na kama wewe una mke au Mume utaona Uzuri wa mumeo,mkeo au Mpenzi wako pale unapomfanya awe huru  kwako.   Utaona kama vile anazidi Kuwa mzuri🤒

5️⃣Na mwisho kabisa...utagundua Kuwa hakuna mtambo mkubwa wa kufyatua mawazo mazuri ya maendeleo kama Nafsi ya mwanadamu iliyowekwa Huru..

Ukisoma Isaya 61:1-5. Anaeleza ..

Roho Wa Bwana Yu juu Yangu.......amenituma kuwatangazia waliofungwa habari za kufunguliwa kwao(kuwekwa huru kwao)

Sasa..kwanini awaweke huru?

Kwa sababu kuna vitu anataka avione vikichanua kutoka kwao hawa waliokuwa wamefungwa

Ukitaka uwe bora...tafuta kwanza uhuru wako...aisee Kuwa huru ni Raha sana

Kila kitu utaona kinaenda pale unapokuwa huru...na kila jambo lazima litaenda tu pale unapokuwa huru...

Ninakutangazia uhuru wako leo Katika Jina la Yesu Kristo
Bwana akuweke huru tena. 

Mwal.Chavala PM Ezekia

Online Gospel Sermons.

Jiunge na Mafundisho yetu kila siku Kwenye magroup yetu ya whatsapp -OGS..

Bonyeza link hii kwa magroup ambayo bado yako wazi
https://chat.whatsapp.com/K3lnh9YaO7Y2Z3SA2MBudI

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.