MAOMBI
🔥ninakusalimia katika Jina la Bwana Yesu
Karibu katika sermon yetu ya siku ya leo
👉🏼wa Kristo wengi tumekuwa na tabia ya kutoomba Mara kwa Mara ,nilikuwa najiuliza ni kwanini, nimepata majibu Haya
1.Maombi ya watu wengi ni Kama huwa hayajibiwi,kwahiyo mtu anaamua kukata tamaa
2.Mtu yeyote huwa anatamani kila anachokifanya kiweze kuleta matokeo SAA ileile,Sasa kuna wakati ukiomba utatakiwa kusubiri,watu wengi hawataki kusubiri ndio sababu wanaacha na kukata tamaa.
*DHANA YA MAOMBI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO*
Mtu anayeomba ni Kama mtu anayepiga ngumi hewani,
Kwa hakika hawezi kuona matokeo kwa macho,lakini katika ulimwengu wa Roho,mtu huyo amepiga molecules nyingi sana za hewa
Tatizo ni kwamba ,hewa huwa haionekani..kwahiyo huwezi kuona umepiga hewa kiasi gani
Lakini endapo hewa ingeweza kuwa inaongea ..basi ingekwambia kwakweli molecules nyingi sana zimepigwa na wewe.
*FAIDA ZA MAOMBI*
1️⃣Maombi huondoa hofu ya ndani(internal fear) kwahiyo unaweza kujiona uko na tatizo kubwa ..lakini unapoenda kuomba kuna namna unaondoa sumu akilini mwako
Ndio maana Wakristo wanaoomba kisaikolojia huwa wako vizuri zaidi ya wale wasioomba
2️⃣Maombi huimarisha mahusiano yetu na Mungu
Mtu yeyote ambaye huwasiliani nae Mara kwa Mara..taratibu mahusiano baina yenu huwa yanakufa
Lakini ukiwa unawasiliana nae Mara kwa Mara ..mahusiano yenu yanakuwa imara sana
3️⃣Maombi hujenga Imani.
Kinachotokea unapotamka Yale maneno katika maombi,akili yako inafanya kazi ya kumemmorise(kujenga kumbukumbu) Sasa ukiendelea sana kuyatafakari yanabadilika yanakuwa vile unavowaza na hatimaye yanakujenga wewe kiimani unakuwa vilevile unavoomba
Ndio maana Biblia inasisitiza maombibya bila kukoma kwa sababu kwa kadri unavoomba sana ndivyo wewe unabadilika nakuwa Yale maombi.
4️⃣Maombi hutia nguvu
*Soma Luke 22:39-46*
Hata Yesu alipewa nguvu za kukabiliana na mate so baada tu ya maombi
Kwa lugha nyingine ..Kama Yesu asingeomba...kazi ya kuelekea ukombozi pale msalabani ingekuwa ni ngumu sana kwake
Ila alipoingia katika maombi ndipo alipata zile nguvu za kukabiliana na mateso
5️⃣Maombi ni Msingi wa kilajambo(Project)
👉🏼
Ninaye ndugu yangu mmoja namuhifadhi kwa jina alikuwa ananisimulia namna Mungu alivyomsaidia kupata mafanikio ya haraka katika maisha yake
💥anasema kila alipokuwa akipanga kufanya jambo ...alikuwa akiingia kwenye maombi kwanza marefu halafu akitoka kwenye Yale maombi project zake zinaenda bila shida
*Kumbuka matahayo 4:1....*.Yesu pia kabla ya kuanza kazi zake hapa Duniani aliamua kujenga Msingi wake katika maombi
Utaona siku ile amemaliza maombi yake siku arobaini alipotoka kule alikuwa na nguvu zisizo za kawaida ndipo akaweza kufanya kazi zote za baba yake
*Wito wangu kwako*
Jifunze kuomba peke yako,omba ukiwa na wakristo wenzako,kwa hakika Hatuna mtu aliyewahi kuingia katika maombi akaomba kwa Imani halafu asijibiwe
Matahayo 7;7 inaeleza tuombe kwakuwa tutajibiwa
*#Munguanajibumaombi*
Endelea kutufwatilia
Mwal.Chavala PM ezekia
Online Gospel Sermons
+255677904755
Facebook..Gospel sermon Ministries,
Kujiunga nasi bonyeza link hii...
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments