MSHINDE GOLIATH WAKO
UJASIRI DHIDI YA GOLIATH
💥Kila mtu ana Goliath wake anaenguruma na kupigapiga kelele sana mbele yake.
👉🏾kitakachokusaidia kupigana nae hatimaye akanyamaza mbele yako ni akili yako
1Samweli 17:32
Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.
Mambo ya kufanya ili kumshinda Goliath wako
*1⃣iambie akili yako kuwa kwa hakika utakwenda kumpiga Goliath.* Ukiweza jisemeshe kwanguvu hadi ujisikie💪🏼
2️⃣Tafuta shuhuda wa pembeni na umwambie huyu Goliath naenda kumpiga
Daudi alimwambia Sauli kama shuhuda na kumhakikishia kuwa i will fight this!
#unaposimualia kwa mwingine ,kuna namna unatengeneza Ujasiri usio wa kawaida
Unadhani kwanini wapiga mieleka huwa wanaanza kwa majigambo ya kuambiana ..nitakutandika wewe. Mbele za watu???
Kuna nguvu kubwa kushuhudia kwa watu jinsi utakavyomtwanga adui yako
3️⃣Mwambie Goliath mwenyewe Directly kuwa unaenda kumpiga kwa Jina la Bwana wa majeshi
👉🏾Kama huwa ukisikia matisho ya shetani dhidi yako...basi na wewe anza kumtisha ...kwa kumwambia utakavyomchakaza...na umchakaze kisawasawa kwa Jina la Yesu
💥Nakuahidi...kwa kufanya hivyo...utamshinda Goliath kama Daudi
#ushindi ni vile umecheza vizuri kete ya saikolojia yako
#Chavala PM Ezekia
Online Gospel Sermons
https://chat.whatsapp.com/Khlliv2TlhV7jsT5DuquhA
No comments